Katika
hali isiyotarajiwa, Athanas Lusesa ambaye ni mzazi wa mwanafunzi
anayesoma katika shule ya msingi Ihulike iliyopo katika kata ya
Ushirombo Wilaya ya Bukombe mkoni Geita amemkataza binti yake kufanya
mtihani wa kumaliza elimu ya msingi .
Mwanafunzi
wa kike aliyezuiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi na mzazi
wake kwa hofu ya kufaulu na kuharibu mipango ya mzazi wake ya kutaka
kumuoza ili apate pesa ya mahari kutoka kwa mwanaume amefahamika kwa
jina la Shija Athanasi(14)wa shule hiyo ya msingi Ihulike.
Afisa
Elimu msingi Wilaya ya Bukombe Shadrack Kabanga amethibitisha kuwepo
kwa tukio hilo na kufuatia tukio hilo alikwenda kituo cha polisi
Ushirombo na kuchukua askari ambao walimkamata mzazi huyo.
Tayari mzazi huyo anashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano zaidi na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Naye
mkuu wa wilaya ya Bukombe Amani Mwenegoha amelaani vikali kitendo hicho
kilichofanya na mzazi huyo kwa lengo la kujipatia mali na kuahidi
kuwashughulikia wazazi wanaozuia jitihada za serikali kuhakikisha mtoto
wa kike anapata elimu.
0 Response to "MZAZI ANAYEPENDA PESA AMKATAZA MTOTO WAKE ASIFANYE MTIHANI WA DARASA LA SABA KISA AOLEWE."
Post a Comment