Habari za hivi Punde

MAFUNZO YALIYOANDALIWA NA MCT KWA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA NA SIMIYU YAMEMALIZIKA LEO MJINI SHINYANGA

Hapa ni ndani ya ukumbi wa Mwalimu House mjini Shinyanga ambapo leo mafunzo ya siku 4 kwa waandishi wa habari 25 kutoka mkoa wa Shinyanga na Simiyu juu ya namna ya kuandika habari katika mazingira hatarishi na maadili ya uandishi yaliyoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania yamemalizika.Aliyesimama ni katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga bi Kareny Masasy ambaye pia ni mwandishi wa gazeti la Habarileo akisoma taarifa ya klabu hiyo kuhusiana na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo waandishi wa habari mkoani humo.Pamoja na mambo mengine aliliomba baraza la Habari Tanzania(MCT)kuendelea kutoa mafunzo wandishi kuhusu mambo mbalimbali.Kushoto ni mwenyekiti wa SPC Shija Felician,wa kwanza kulia ni Mwakilishi MCT bwana Paul Mallimbo


Mwakilishi  Baraza la Habari  Tanzania Paul Mallimbo akitoa hotuba fupi baada ya mafunzo ya siku 4 kwa waandishi wa habari kumalizika leo.Mallimbo alisema MCT imeamua kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari nchi nzima kuhusu namna ya kuripoti habari katika mazingira hatarishi na maadili ya kazi yao ili kuwajengea uwezo ili waripoti vizuri habari zao kwa usalama zaidi na kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazima.Alisema MCT inalengo la kuwafikia waandishi wa habari 350 na mpaka sasa wamewapatia mafunzo hayo waandishi wa habari 275.


Baada ya mafunzo hayo washiriki wote walipatiwa vyeti vya ushiriki,kushoto ni mwandishi wa habari kutoka Radio Faraja Moshi Ndugulile akipokea cheti cha ushiriki wa mafunzo hayo.Mafunzo hayo yalikuwa ya nadharia na vitendo


Kushoto ni mwandishi wa habari Star Tv/RFA Shaban Alley kipokea cheti cha ushiriki wa mafunzo na kushikana mkono na Mwakilishi  Baraza la Habari  Tanzania Paul Mallimbo 


Kushoto ni bwana Kadama Malunde ambaye sasa ni mwandishi wa habari gazeti la Zanzibarleo na mkurugenzi wa Malunde1 Blog akipokea cheti cha ushiriki wa mafunzo hayo na kushikana mkono na Mwakilishi  Baraza la Habari  Tanzania Paul Mallimbo 


Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga bwana Shija Felician ambaye pia ni mwandishi wa habari gazeti la Mwananchi akifunga mafunzo ya siku 4 kwa waandishi wa habari ambapo aliwataka washiriki wa semina hiyo kuyafanyia kazi yote waliyojifunza huku akiiomba MCT kuendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari.

ANGALIA PICHA ZINGINE HAPA
KARENY. Powered by Blogger.