Habari za hivi Punde

SABABU YA KUFARIKI KWA WATOTO MAPACHA HOSPITALI YA MKOA NESI AWAJIBIKA KWA UTENDAJI MBOVU.

Mamia ya wakazi wa Shinyanga wakiwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga usiku huu,nje ya wodi namba 8 ya wazazi wakifurahia waandishi kufika eneo la tukio,ambapo jioni hii kumetokea sereka la aina yake baada ya nesi mmoja(Jina tunalo) ambaye amedaiwa kusababisha vifo vya watoto wawili mapacha,inadaiwa kuwa mama mjamzito kafikishwa hospitalini hapo kwa ajili ya kujifungua lakini nesi aliyekuwepo alikuwa bize na simu ya mkononi bila kumjali/kumpatia huduma yoyote pamoja na kuombwa na ndugu zake na mama huyo kuwa tayari alikuwa ameanza kupush matokeo yake watoto wote wakafariki dunia.Inaelezwa kuwa nesi alikuwa yuko bize na simu ya mkononi akichat

Bi  Mwanaisha Juma mkazi wa Mshikamano mjini Shinyanga Mama mzazi wa mama aliyefikishwa hospitalini hapo,akizungumza na waandishi wa habari walifika eneo la tukio ambaye alisema amemfikisha mwanaye  Zena Pius kujifungua  tangu saa 6 na nusu mchana leo na (Uchungu)dalili za kujifungua zimeanza saa 7 na ilipofika saa 10 wakiwa hospitalini hapo wodi namba 8 alianza kupush wakaomba msaada kwa manesi waliokuwa zamu lakini hakuna aliyejali matokeo yake watoto wakafariki dunia saa 10 na nusu.Kwa mujibu wa mama huyo nesi aliyewa zamu alikuwa bize na simu takribani nusu saa hadi akaja nesi mwingine kutoa msaada 

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo la aina yake akizungumza na waandishi wa habari usiku huu

Waandishi wa habari wakiwa kazini eneo la hospitali ya mkoa wa Shinyanga usiku huu

Waandishi wa habari wakiwa nje ya ofisi ya mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Fredrick Mlekwa ,ili kujua undani wa tukio hilo,ingawa hata  hivyo baada ya kumsubiri muda wa takribani nusu saa akizungumza na nesi huyo ofisini kwake,nesi huyo alitoroshwa na baada ya kuingia ofisini,aliwaambia waandishi wa habari kuwa  yeye siyo msemaji,msemaji ni mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dkt Ntuli Kapologwe na kwamba taarifa kamili itatolewa kesho asubuhi kwani bado wanafuatilia undani wa tukio hilo

Nesi anayetuhumiwa kusababisha vifo vya watoto wawili mapacha akitoroshwa hospitalini akiwa amejifunika nguo ili waandishi wasimpige picha
Gari lililotumika kumtorosha mtuhumiwa,siti ya nyuma akiwa amejifunika nguo

Picha zote na Mwandishi Maalum wa Malunde1 blog
KARENY. Powered by Blogger.