Kumbukumbu zako ziko sawa kuhusu yale malalamiko ya kukosewa kwa
picha ya Mwalimu Nyerere kwenye noti ya shilingi elfu moja? basi kama
hazipo sawa, ichukue hiyo.
Baada ya hayo malalamiko unaambiwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),
imesema imeanza kufanyia kazi malalamiko ya kukosewa kwa picha ya Rais
wa kwanza wa Tanzania,
Marehemu Mwalimu Julius Nyerere ambapo mkurugenzi
wa huduma za kibenki Emmanuel Boaz amesema tayari benki hiyo imeanza
kufanyia kazi hayo malalamiko baada ya kusoma katika mitandao ya jamii.
Mwananchi wameandika mkurugenzi
huyo alisema BoT haijapata taarifa rasmi kutoka kwa mtu yoyote lakini
wameamua kuzifanyia kazi taarifa hizo >>>“Na
sisi tumesoma katika mitandao, hakuna taarifa rasmi tuliyoipata lakini
hatuwezi kudharau tuhuma hizo na endapo tukigundua kuna matatizo
tutachukua hatua za kubadilisha haraka”
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, suala la picha kukosewa sio geni kwani
ilishawahi kutokea mara kadhaa kwa marais wastaafu na BoT ililazimika
kubadili haraka ili kutoharibu mtazamo wa Taifa ambapo alitoa mfano wa
picha ya Mwalimu Nyerere kukosewa na kuonekana nguo aliyovaa imefanana
na blauzi lakini pia picha ya Rais Ally Hassani Mwinyi ambayo ilionekana
shingoni ana mikunjo.
Kutokana na hali hiyo, mkurugenzi huyo aliwatoa hofu Watanzania kuwa
endapo itabainika kama noti hizo zina kasoro zitarekebishwa ambapo hivi
karibuni, mitandao ya kijamii iliwakariri wanafamilia ya Rais huyo wa
kwanza wakilalamikia picha hiyo kwenye noti ya Sh1,000 kukosewa.
0 Response to "BOT KUTOA NOTI YA SHILINGI 1000 NI BAADA YA MALALAMIKO KUTOKA KWENYE FAMILIA YA HAYATI BABA WA TAIFA."
Post a Comment