Bunda la mkosi limeendelea kuiandama Simba baada ya kulazimishwa tena
sare ya bao moja kwa moja na maafande wa Prisons katika Uwanja wa
kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya wakati mahasimu wao Yanga wakipata
ushindi mnnono wa 3-0 dhidi ya Stand United mjini Shinyanga.
Yanga imefikisha pointi kumi baada ya kucheza michezo mitano na
kuwacha mahasimu wa Simba nyuma kwa pointi tano baada ya kupata sare
yake ya tano kutokana na michezo yake mitano.
Tofauti na furaha na nderemo za Wanajangwani, Simba mambo si shwari,
kwani matekeo haya mabaya sana tangu kuanzishwa kwake kwa kuambulia
pointi tano kutokana na mechi tano ambayo yanaifanya timu hiyo kupoteza
jumla ya pointi kumi tangu kuanza kwa msimu huu wa Vodacom Premier
League.
Ilionekana kama Simba ingepata ushindi wake wa kwanza jijini Mbeya
baada ya kuongoza kwa kipindi kirefu, lakini ndoto yao ilikatishwa
katika dakika za majeruhi baada ya Prisons kusawazisha.
Simba ilipata bao la kuongoza kupitia kwa Mganda Emanuel Okwi kabla
ya Prisons kuchomoa dakkika za majeruhi kupitia kwa Hamisi Mahingo.
Tofauti na matokeo ya Mbeya, Yanga imeweza kupata ushindi wake wa kwanza mnono.
Mbrazil Geilson Jaja alifungua ukurasa wa mabao katika dakika ya 13 kwa bao ambalo lilidumu hadi mwisho wa kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili Yanga iliongeza kasi na kuweza kupata mabao mawili zaidi kupitia kwa Jerryson Tegete katika za 77 na 90.
Matokeo mengine ya kushangaza ni kuwa Azam wameonja uchungu wa
kufungwa baada ya kuzabwa bao 1 kwa bila na JKT Ruvu katika uwanja wake
wa Chamazi.
Bao la Samuel Kamuntu katika dakika ya 44 ndilo lililoizamisha Azam na kuifanya ione adha ya kufungwa kwa mara ya kwanza.
Kutoka Mlandizi mkoani Pwani, mwandishi wetu anaripoti kuwa wenyeji
Ruvu Shooting imewachapa maafande wa Polisi Morogoro kwa bao moja kwa
bila katika mchezo mkali uliojaa upinzani.
Alikuwa ni Kassim Daby aliyewainua Ruvu Shooting baada ya kupachika
bao la ushindi katika dakika ya 68 baada ya kuunganisha kimiani mpira wa
kona iliyopigwa kiustadi na Hamisi Nguya.
Mpira uliimalizika katika dakika 45 za kwanza kwa sare ya kutofungana
kabla ya wenyeji kujipatia bao la ushindi dakika 23 baada ya kuanza kwa
kipindi cha pili.
0 Response to "TIMU YA YANGA YAZIDI KUNG'ARA NI BAADA YA KUIBUKA NA USHINDI MNONO WA MABAO 3-0 DHIDI YA STEND UNITED YA MKOA WA SHINYANGA"
Post a Comment