hapa ni mahali pa ofisi ya chadema kwa mkoa wa Shinyanga.
Uchaguzi wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,wilaya ya Kahama mkoani
Shinyanga umeingia dosari,baada ya mmoja wa madiwani wa chama hicho kuhusishwa
na rushwa na vitendo vya usaliti ndani ya chama kutoka CCM.
Pia katika uchaguzi huo
baadhi ya wagombea wamechapana makonde baada ya kuenguliwa kwa baadhi ya
majina ya wagombea katika uchaguzi wa Baraza la Vijana wa chama hicho
(BAVICHA),huku Red Brigade wakihusika katika vurugu hizo.
Hali hiyo ilitokea juzi
mjini Kahama katika ukumbi wa Mamba Hall, baada mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti
wa Chama hicho wilayani Kahama Leonard Mayala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya
Nyasubi, alienguliwa kuwania nafasi hiyo baada ya kubainika kutumia rushwa
kuomba achaguliwe katika nafasi hiyo.
Mgombea huyo alituhumiwa
kutumia shilingi milioni mbili kuwahonga baadhi ya wanachama,fedha ambazo
zinadaiwa zilitolewa na baadhi ya makada wa Chama cha Mapinduzi kwa njia ya
mtandao wa (Mpesa)ili kuhakisha ananyakuwa nafasi hiyo.
Tuhuma hizo
zimekuja baada ya wanachama kutokuwa na imani naye kutokana na
mwenendo wa diwani huyo wa kuwa karibu na makada wa CCM wilayani hapa na hivyo
kusababisha viongozi na wasimamizi wa uchaguzi huo kuengua jina lake
baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na kuwekewa pingamizi.
Aidha katika uchaguzi
huo baadhi ya wagombea na wanachama walichapana makonde wakipinga kuenguliwa
majina ya baadhi majina ya wagombea katika uchaguzi wa Baraza la Vijana
wa Chadema (BAVICHA).
Ugomvi huo ulitokea
baada ya wagombea waliopitishwa katika nafasi ya Uenyekiti wa Bavicha
kuanza kujinadi kwa wananchama ndipo mgombea Thomas Masanja aliyeenguliwa
katika kinyang’anyiro hicho kutokana na kukosa sifa ikiwemo kadi yake ya
uanachana kutotambulika alijitokeza na kuzuia uchaguzi.
Kufuatia kuenguliwa kwa
mgombea huyo ndipo badhi ya wafuasi wake wakiwemo Red Brigade
walipojitokeza na kuanza kufanya fujo kwa lengo la kuzuia uchaguzi huo
kuendelea wakidai kwamba mgombea wao kutotendewa haki kwa kuenguliwa kinyemela
kugombea nafasi hiyo.
Hali hiyo ilikwenda
mbali zaidi kwani wafuasi hao walianza kuwashambulia baadhi ya viongozi
na wasimamizi ambapo Mwenyekiti wa Chadema wa Halmashauri ya Msalala
Emmanuel Bombeda alipigwa ngumi na Red brigade waliokuwa wakimuunga mkono
mgombea aliyeenguliwa.
Utulivu na amani urejea
ukumbini humo baada ya msimamizi wa uchaguzi wa Chama hicho kanda ya Ziwa
Mashairiki,Madata Sande kuingilia kati na kuwataka wanachama kuwa
wavumilivu ili kufanikisha uchaguzi huo kwani wagombea walioenguliewa katika
kinyang’anyiro hicho walienguliwa kihalali bila upendeleo wowote kwa
kuzingatia katiba ya chama hicho.
Katika uchaguzi
huo wajumbe walimchagua Juma Protas,kuwa Mwenyekiti wa Chadema wa
wilaya hiyo,naye Mshibu Peter akiteuliwa kushika nafasi ya Ukatibu wa chama
hicho,nafasi ya Ukatibu Uenezi ikimwangukia Anord Peter na Mweka Hazina
alichaguliwa,Elias Mayunga.
Nalo Baraza la Vijana
BAVICHA lilimchagua Samwel Peter kuwa Mwenyekiti wake na ndani ya uchaguzi huo
wajumbe walichagua viongozi mbali mbali wa yakiwemo mabaraza ya
Wazee,Wanawanake na wajumbe wa mkutano mkuu taifa wa chama hicho.
via>>mohabmatukio
blog
|
0 Response to "WANAO WANIA UONGOZI NDANI YA CHADEMA WILAYANI KAHAMA MKOANI SHINYANGA WATWANGANA MAKONDE"
Post a Comment