WAKATI JANA ni mwisho wa ukamilishaji wa madawati mkoa wa Shinyanga umeshindwa
kukamilisha agizo la Rais John Magufuli la kutatua
tatizo la uhaba wa Madawati kwa shule za msingi na sekondari ambapo bado
inakabiliwa na upungufu wa madawati 9,545
Akitoa takwimu
hizo juzi Ofisa Elimu taaluma mkoa James Malima alisema katika shule za msingi kuna upungufu wa
madawati 7,310, sekondari 2,235 na kufanya jumla kuu kuwa ni 9,545 huku
utengenezaji wa madawati hayo kwenye halimashauri bado ukiendelea ambapo badhi
yao zimeshavuka lengo.
Aidha Malima
ametaja halmashauri ambazo zimetekeleza agizo hilo la Rais Magufuli la kumaliza
tatizo la uhaba wa madawati kuwa ni halmashauri ya mji wa kahama, na msalala ambazo
zImemaliza tatizo hilo kwa shule zote za msingi na sekondari.
Pia Malima
amezitaja halmshauri za Ushetu ambayo imekamilisha tatizo la madawati kwa shule
za sekondari pekee, huku shule za msingi ikiwa na upungufu wa madawati 387, shinyanga
manispaa nayo ikabiliwa na uhaba wa madawati 2,033 kwa shule za msingi ambapo
sekondari imeshatekeleza agizo hilo.
Hata hivyo
amezitaja halmashauri mbili ambazo hazijatekeleza agizo hilo kwa shule zote
kuwa ni kishapu ambapo shule za msingi inakabiliwa na uhaba wa madawati 2,112,sekondari
1,965, Shinyanga vijijini msingi 2,778,sekondari 270 na hivyo kufanya mkoa kuwa
na upungufu wa madawati 9,545.
Rais Magufuli
alitoa agizo hilo la kukamilisha uhaba wa madawati kwa shule zote nchini ambapo
mwisho wa kukabidhi madawati hayo ilipangwa kuwa leo huku mkoa wa Shinyanga ukishindwa
kutekeleza agizo hilo.