Habari za hivi Punde

MWANAUME AJINYONGA KWA KUTUMIA CHANDARUANa  Kareny  Masasy
Shinyanga.
MWANAUME  Njile Nkelembi anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka (55) mkazi wa kijiji cha Maskati kata ya Imesela katika wilayani  Shinyanga  mkoani hapa   amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia chandarua katika mti wa mwembe katika shamba lake.
Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamewaeleza  waandishi wa habari kuwa  mnamo majira ya  saa moja na nusu asubuhi  jana katika kitongoji cha Kitunda  kwenye eneo la  Maskati  walikuta  mwili wake ukiwa unaning’inia  juu ya mti huo.
Aidha  mwenyekiti wa  kijiji cha Maskati  Hamis Salum amesema  hadi sasa hakuna sababu iliyopelekea kutokea kwa kifo hicho kwani hapakuwa na ugomvi wowote katika familia yake.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Imesela Juma Kayumbo ameeleza kuwa  kusikitishwa na taarifa ya kifo hicho na kuongeza kuwa chanzo cha kifo hicho bado hakijajulikana waziwazi kwani marehemu hakuacha ujumbe wowote.
Kamanda wa polisi mkoa waShinyanga  Evarist Mangala amesema  bado hajapata taarifa kuhusu tukio hilo kwani hakuna ndugu wala jamaa aliyetoa taarifa kwa jeshi la polisi kuhusu tukio hilo.KARENY. Powered by Blogger.