Habari za hivi Punde

UONGOZI WAAGIZWA KUUNDA KAMATI MAALUMU YA KUTEMBELEA MAENEO YALIYOVAMIWA.



 Na  Kareny  Masasy
Simiyu.
 
UONGOZI  mkoani  Simiyu umeagizwa kuunda kamati maalumu itakayotembea halmashauri zote mkoani hapa kukagua na kuchunguza maeneo yaliyovamiwa na wananchi katika shule za msingi na sekondari, zahanati pamoja na vituo vya afya, ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Sambamba na agizo hilo aidha katika kamati hiyo maalumu itakayoundwa na uongozi wa mkoa imeagizwa kuchunguza wale wote waliohusika kutoa maeneo hayo ya serikali kwa kuchunguza idara za ardhi katika Halmshauri hizo, na watakao bainika watafukuzwa kazi pamoja na kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria.

Agizo hilo limetolewa na Naibu waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa TAMISEMI Agrey Mwanri wakati akifanya majumuisho wilayani itilima katika mwendelezo wa ziara yake ya kikazi wilayani humo.

Mwanri alimtaka Katibu Tawala wa Mkoa Mwanvua Jilumbi kuunda kamati hiyo haraka iwezekavyo, kutokana na maeneo mengi katika wilaya hiyo kuonekana yamevamiwa na watu, mtu binafsi, pamoja na viongozi wengi kujichukulia uhamuzi wa kujipatia maeneo hayo bila ya kufuata uutaratibu.

“Nataka kuagiza hapa katibu tawala wa mkoa ndani ya siku chache kabla sijahitimisha ziara yangu hii, unda kamati ya watu wachache watakao kwenda katika kila wilaya mkoa mzima, wachunguze waliogawa maeneo hayo bila ya kufuata utaratibu, waliovamia pamoja na waliaojigawia maeneo hayo ambayo ni ya serikali na wachukulie hatua za kisheria haraka iwezekanavyo”Alisema Mwanari.

Aidha katika hatua nyingine Naibu waziri huyo aliapiga marufuku mahakama za kimila (Dagashida), baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo Gorgina Bundara kumtaka Naibu huyo kuwasaidia katika kupambana na jambo hilo.

Alisema kuwa mila hiyo imeonekana ikikiuka miiko yake kwa kuonekana kuingilia masuala ya serikali, kutokana na kujichukulia hatua za kisheria mikononi, ambapo aligiza wale wote wanaohusika kuendesha mahakama hizo kukamatwa mara moja na kuchukuliwa hatua za kisheria.





0 Response to "UONGOZI WAAGIZWA KUUNDA KAMATI MAALUMU YA KUTEMBELEA MAENEO YALIYOVAMIWA."

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.