Na Kareny Masasy
Simiyu.
Uongozi wa mkoa wa Simiyu umeagizwa kuunda kamati maalumu
itakayotembea halmashauri zote mkoani hapa kukagua na kuchunguza maeneo
yaliyovamiwa na wananchi katika shule za msingi na sekondari, zahanati pamoja
na vituo vya afya, ili wachukuliwe hatua za kisheria.
Sambamba na agizo hilo aidha katika kamati hiyo maalumu
itakayoundwa na uongozi wa mkoa imeagizwa kuchunguza wale wote waliohusika
kutoa maeneo hayo ya serikali kwa kuchunguza idara za ardhi katika Halmshauri
hizo, na watakao bainika watafukuzwa kazi pamoja na kuchukuliwa hatua nyingine
za kisheria.
Agizo hilo limetolewa na Naibu waziri wa Tawala za Mikoa na
Serikali za mitaa TAMISEMI Agrey Mwanri wakati akifanya majumuisho wilayani
itilima katika mwendelezo wa ziara yake ya kikazi wilayani humo.
Mwanri alimtaka Katibu Tawala wa Mkoa Mwanvua Jilumbi kuunda
kamati hiyo haraka iwezekavyo, kutokana na maeneo mengi katika wilaya hiyo
kuonekana yamevamiwa na watu, mtu binafsi, pamoja na viongozi wengi
kujichukulia uhamuzi wa kujipatia maeneo hayo bila ya kufuata uutaratibu.
“Nataka kuagiza hapa katibu tawala wa mkoa ndani ya siku
chache kabla sijahitimisha ziara yangu hii, unda kamati ya watu wachache
watakao kwenda katika kila wilaya mkoa mzima, wachunguze waliogawa maeneo hayo
bila ya kufuata utaratibu, waliovamia pamoja na waliaojigawia maeneo hayo
ambayo ni ya serikali na wachukulie hatua za kisheria haraka
iwezekanavyo”Alisema Mwanari.
Aidha katika hatua nyingine Naibu waziri huyo aliapiga
marufuku mahakama za kimila (Dagashida), baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo Gorgina
Bundara kumtaka Naibu huyo kuwasaidia katika kupambana na jambo hilo.
Alisema kuwa mila hiyo imeonekana ikikiuka miiko yake kwa
kuonekana kuingilia masuala ya serikali, kutokana na kujichukulia hatua za
kisheria mikononi, ambapo aligiza wale wote wanaohusika kuendesha mahakama hizo
kukamatwa mara moja na kuchukuliwa hatua za kisheria.
0 Response to " "
Post a Comment