Na Kareny Masasy
Shinyanga
SHIRIKA lisilo la kiserikali PACESHI linalotoa msaada wa
kisheria mkoani Shinyanga limetoa mafunzo kwa wasaidizi 25 ambao watasaidia
kufikisha elimu ya kisheria katika jamii iliyoko maeneo ya vijijini ili waweze
kupata haki zao za msingi zinazoelekea kupotea ama zilizopotea.
Akitoa mafunzo hayo mkurugenzi wa shirika hilo jana Perpetua
Magoke alisema mafunzo hayo yatawasaidia kutoa elimu katika jamii zilizoko
kijijini zinazogusa maslahi ya kifamilia kijamii, pamoja na migogoro ya
ardhi.
“Watu wengi hasa walioko katika maeneo ya vijijini hawazijui
haki zao za kisheria hivyo tumeona kuanzisha mafunzo haya kwa watu 25 kila
wilaya ili waweze kufikishiwa elimu ambayo itasaidia wananchi kuondokana na
migogoro mbalimbali inayojitokeza”Alisema Magoke.
Alisema wanawake wamekuwa wakikosa fursa ya kurithi mali
wakati mme akifa hivyo waliopata mafunzo hayo watasaidia kutoa elimu na kuweza
kuzijua sheria na kuondoa migogoro ya urithi ili kuweza kukuza uchumi wao
binafsi.
Kwa upande wake afisa mipango mahusiano na mafunzo John
Shija alisema jamii ikipata elimu itasaidia kuondoa ukatili wa kijinsia katika
makundi, mbalimbali yakiwemo ya wanawake ,watoto,walemavu, wazee,watu wanaoishi
na virusi vya ukimwi pamoja na masikini wa kipato.
Shija alisema makundi hayo yamekuwa yakiathilika sana
kulingana na mazingira wanayoishi katika jamii hivyo ambapo shilika la PACESHI
linajaribu kuamsha mambo ambayo yatalinda maslahi yao.
“Shirika letu linashughulikia mambo mbalimbali zikiwemo
sheria za makosa ya jinai kanuni ya adhabu,sheria zinazohusu mirathi , sheria
za ndoa, sheria ya kudhurumiwa sheria za kudhibiti ukimwi, na sheria mbalimbali
zitakazosaidia jamii zikifanikiwa makundi haya ya takuwa salama
kiulinzi”alisema Shija.
“Pia tunajaribu kuangalia sheria za ardhi zinaoweza
kuwalinda wananchi wakizijua sheria hizo ambazo zimekuwa ni tatizo kubwa katika
jamii itasaidia kupunguza migogoro iliyokithili ambayo inasababisha watu wengi
kukatana na mapanga”aliongeza Shija.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Antony Salamba
alilishukru Shirika la PACESHI kwa kuanzisha mafunzo hayo kwani itasaidia
kuondoa changamoto za migogoro mbalimbali zinazojitokeza katika maeneo ya
vijijini kwani wataenda kutoa elimu na kuweza kutoa ushauri kwa wanakijiji.
Mafunzo hayo yaliyowahusisha washiriki 25 kutoka
katika kata mbalimbali katika wilaya ya Shinyanga yanaendelea kufanyika katika
ukumbi wa Diamond Hotel mjini Shinyanga yatafanyika kwa siku 25 .
Mwisho.
0 Response to "PACESHI YATOA MAFUNZO KWA WASAIDIZI WA KUFIKISHA ELIMU YA KISHERIA KWENYE MAENEO YA PEMBEZONI"
Post a Comment