Na Kareny Masasy
Shinyanga.
MELEZWA kuwa asilimia 70 ya wafanyakazi wa
Migodi hufukuzwa kazi kinyume cha sheria na wawekezaji wa nje ya nchi
wanaowekeza katika sekta ya Madini
Hayo yameelezwa na Hassan
Amir katibu mkuu taifa wa Chama cha wafanyakazi wa Migodi, Nishati
na Ujenzi (TAMICO) alipokuwa
akihuhutubia mkutano mkuu maalumu kanda ya Shinyanga uliofanyika mjini hapa.
Amir amesema Uongozi
wa Migodi ambao unaongoza kuwafukuza wafanyakazi wake ni pamoja na Bulyanhulu
na Buzwagi ambapo kwa kipindi cha januari hadi disemba mwaka huu zaidi ya
wafanyakazi 80 walifukuzwa kazi kinyume cha sheria za kazi.
Akifafanua amesema katika mgodi wa Bulyanhulu pekee wafanyakazi
50 walifukuzwa kazi na katika mgodi wa Buzwagi wafanyakazi 35 walifukuzwa kazi
baada ya afya zao kuzorota baada ya kuugua kutokana na madawa mbalimbali yenye
sumu ambayo hutumika migodini.
Amesema katika
kipindi cha mwaka 2013 kesi 70 zilifunguliwa katika ofsi za idara ya kazi na
kesi zingine 15 zimefunguliwa mahakama kuu za hapa nchini huku zikisimamiwa
na tamico na kupata ushidi.
Wakati huohuo wajumbe
wa mkutano huo ulimchagua Antony Masonda
kuwa mwenyekiti wa kanda ya Shinyanga na Clioford Wambura alichaguliwa kuwa
mjumbe wa baraza kuu la Taifa.
Katika nafasi ya Mwenyekiti wa kamati ya vijana wa kanda
alichaguliwa Pius Mashimba wakati Shija Golani na
Vaileth Matanga walichaguliwa kuwa wajumbe wa kamati ya utendaji kanda ya
Shinyanga.
0 Response to "ASILIMIA 70 YA WAFANYAKAZI MGODINI HUFUKUZWA KAZI KINYUME CHA SHERIA YA SEKTA YA MADINI NCHINI."
Post a Comment