IMEELEZWA kuwa vifaa tiba na madawa huchelewa kuwafikia
katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga hali
ambayo imepelekewa wagonjwa kupata
changamoto ya ukosefu wa dawa hospitalini hapo.
Hayo yameelezwa na mganga mfawithi wa hospital hiyo Dkt Fredrik Mlekwa wakati akiongea na waandishi wa habari jana
hospitalini hapo baada ya kupata
malalamiko ya wagonjwa kukosa dawa
ikiwemo vifaa tiba.
Hata hivyo amesema
kuwa katika suala hilo aliiomba Serikali
kuangalia upya utaratibu wake wa
kusambaza madawa pamoja na vifaa tiba viweze kufika kwa muda muafaka,
Aidha amesema kuwa kitengo cha bohari ya dawa
MSD kilichopewa jukumu la kusambaza wamekuwa wakichelewa kufikisha na pia
kuleta vifaa ambavyo hawaku agizwa..
Amesema kumekuwa na changamoto nyingi za madawa na
vifaa tiba pamoja na serikali kila baada ya bajeti kupita wizara hupelekwa fedha MSD kwa ajili ya vifaa tiba na madawa ambapo haviji kwa muda muafaka.
Akiitupia lawama MSD
anasema kuwa uwezo wao
wakusambaza dawa ni asilimia 25 au 30 na asilimia inayobaki hununua dawa kutokana na upatikanaji wa vyanzo vya Hosptalini hapo.
Amesema kutokana
na changamoto hizo viongozi huandaa mahitaji na kupeleka mkoani kitengo cha
manunuzi kwa ajili ya kutangaza tenda ya mahitaji ya madawa na ndio mzunguko
huo hujenga malalamiko toka kwa
wagonjwa madawa yanapo adimika.
0 Response to "TATIZO SIO HOSPITALINI BALI BOHARI ZA DAWA HUCHELEWESHA"
Post a Comment