Na Kareny Masasy
Itilima.
NAIBU waziri wa
tawala za mikoa na serikali za mikoa Agrey Mwanri amemsimamisha kazi Kaimu
mhandisi wa halmashauri ya Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu,Paschal Manyama
baada ya kubainika mradi wa barabara inayoingia kwenye ofisi ya Halmshauri hiyo
yenye kilometa 1.03 kuwa chini ya kiwango.
Hatua ya kusimamishwa kazi kwa mhandisi huyo ilikuja
wakati waziri huyo alipotembelea mradi
wa ujenzi wa barabara hiyo iliyokuwa chini ya Mkandarasi Virgin Company
Limited, iliyokuwa imejengwa kwa gharama ya kiasi cha shilingi Milioni 9.01 wakati wa
mwendelezo wa ziara yake wilayani humo.
Akikagua mradi huo Mwanri alibaini ujenzi huo kufanyika
chini ya kiwango kwa kutokuwepo kwa mitaro ya kutolea maji, ambapo mhandisi
huyo alipoulizwa juu ya jambo hilo ilishindwa kutoa majibu ya kuridhisha.
Wakati akiendelea kukagua mradi huo mwanri alibaini kuwepo
kwa kasoro nyingi katika ujenzi huo, baada ya kubainika mkandarasi aliyepewa
kazi ya ujenzi huo, kutopewa mkataba, pamoja na mchoro unaonyesha gharama za
mradi (BOQ) kutokuwepo.
Hatua hiyo ilimpelea Naibu waziri kuwa na mashaka na
mhandisi huyo kutokana na majibu aliyokuwa akitoa kutokua ya kitaalamu, hali
iliyomlazimu kumuuliza Mhandisi huyo kiwango chake cha elimu.
Alipoulizwa elimu yake Mwahandisi Manyama alisema alimu yake ni kidato cha nne,
jambo lilomfanya Naibi waziri kumwagiza Katibu Tawala wa Mikoa Mwanvua Jilumbi
kumwondoa katika nafasi ya Uhandisi na badala yake atafutiwe kazi mbadala
tofauti na hiyo.
“Natoa agizo Mhandisi huyo namsimamisha kazi hafai hata
kidogo kuwa katika nafasi hii, ndiyo maana nauliza maswali yanamshinda na kama
ataendelea kukaa hapa halmashauri itapata hasara kubwa, sasa namsimamisha kazi,
Katibu tawala wa mkoa tafuta mtu mwingine umweke hapa, huyu hafai hata kidogo mtafutie kazi
nyingine”Alisema Mwanri.
Hata hivyo ilibanika kuwa mhandisi huyo anakaimu nafasi hiyo
kutokana na Hamlshauri kutokuwa na Mhandisi wa ujenzi, ambapo waziri alimpa muda wa masaa 24 kuleta vyeti vyake kama kweli alisomea mambo ya ujenzi.
0 Response to "MHANDISI HALMASHAURI YA ITILIMA ASIMAMISHWA KAZI NA NAIBU WAZIRI TAMISEMI"
Post a Comment