Na Kareny Masasy
Shinyanga.
Zaidi ya Shilingi
millioni 287 zilitolewa na serikali kuu katika bajeti ya fedha ya mwaka 2012/13 ikiwa ni mpango wa kuendeleza miradi ya majengo ya shule za
msingi ,nyumba za walimu katika
halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
ambapo shule ya msingi Ihugi kata ya Lyamidati imelalamikiwa kupata
fedha pungufu na kiasi
kilichotengwa.
Hayo yamesemwa
jana na diwani Leo Mayiku
kutoka kata hiyo wakati akiongea
na waandishi wa habari mjini Shinyanga huku akieleza kuwa shule hiyo ilipata
kiasi cha shilingi millioni 16.5 kwaajili ya kuendeleza mradi wa madarasa
matatu .
Alisema kuwa licha ya
kutengewa fedha hizo kiasi cha zaidi ya
shilingi lakini nne zimeonekana kutolewa
na kushindwa kuelewa zimekwenda wapi huku akidai kuwa pesa hizo ni nyingi
zingeweza kuendeleza ujenzi mwingine unaohitajika shuleni hapo.
“Mimi kama diwani nitahakikisha nafuatilia fedha hizo
zilichukuliwa na kwenda wapi ikiwa niliwauliza wahusika waliokwenda kuchukua
benki na kuonyesha maelezo ya
risiti ambao ni mkuu wa shule hiyo
Mesoya na mwenyekiti wa kamati ya shule
Leonadi Gwangutebe wakidai walichukua
na kukuta kiasi cha fedha hicho.”alisema Diwani.
Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo Ayoub Mesoya alisema
kuwa wao walipokea kiasi ambacho
walichokikuta benki hawakufahamu
mapungufu yaliyojitokeza ila
walimuelezwa diwani kiasi cha fedha walichokitoa benki na vielelezo vyote ambapo ilikuwa imekosekana zaidi ya shilingi laki nne.
Pia alisema kuwa mpaka sasa kuna uhaba wa vyoo vya walimu na
matundu ya vyoo vya wanafunzi kwani matundu yaliyopo kwa upande wa wanafunzi ni
manne ambayo hayatoshelezi huku walimu
wakikosa choo na kwenda kupata huduma hiyo katika choo cha familia ya mwalimu
mkuu.
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri hiyo Kiyungi Mohamedi alisema
kuwa malalamiko hayo ameyasikia kutoka
kwa diwani ambapo halmashauri inachukua jukumu la kukagua fedha zote zilizoingizwa katika kuendeleza miradi ya shule za msingi ili kuona mapungufu
yaliyojitokeza kama ni sahihi kweli kupata kiasi hicho.
Ambapo Kiyungi
alisema kuwa jumla ya shule za msingi 32 zilitengewa kiasi cha zaidi ya shilingi millioni 287 katika bajeti yake ya kipindi cha mwaka
2012/13 kwa lengo la kukamilisha majengo
ya shule
pamoja na nyumba za walimu yaliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi.
0 Response to "DIWANI ALALAMIKA KUPUNJWA KWA FEDHA ZILIZOTOLEWA KWAAJILI YA MRADI WA KUENDELEZA MAJENGO MATATU YA SHULE YA MSINGI IHUGI"
Post a Comment