Bariadi. Matukio ya kuuawa kwa watu wenye ulemavu wa Ngozi (Albino)
yamezuka upya mkoani Simyu, ambapo mwanamke mmoja Mughu Lugata (40) mwenye
ulemavu wa ngozi (Albino) ameuawa kinyama kwa kukatwa katwa mapanga na watu
wasiojulikana pamoja na kutoweka na baadhi ya viungo vyake.
Tukio hilo lililotokea
katika kitongoji cha chalala kijiji cha Gasuma kata ya Nkololo wilayani Bariadi
Mkoani hapa, marehemu alikatwa mguu wake wa kushoto sehemu ya goti, vidole 2
mkono wa kushoto pamoja ukucha wa kidole gumba , ambapo wahusika walitoweka na
viungo hivyo.
Akitoa taarifa mbele za
waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa polisi mkoani hapa Charles Mkumbo
alisema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa 12 usiku hadi saa
moja hasubuhi,wakati marehemu akiwa nyumbani kwake.
“marehemu aliuawa na
kiungo chake cha mguu wa kushoto kuchukuliwa kwa kukatwa sehemu ya goti, vidole
2 vya mkono wa kushoto ambavyo ni kidole cha 3 na 4,kukatwa na kuchuliwa na
ukucha wa kidole gumba cha mkono wa kushoto na viungo vyote hivyo vilitoweka na
wahusika wa mauaji hayo” Alisema Mkumbo.
Alisema kuwa akiwa
amelala nyumbani kwake peke yake mwasnanmke huyo alivamiwa na watu
wasiojulikana na kuanza kumkatakata mapanga na kuchukua baadhi ya viungo vyake
vya mwili na kutokomea navyo kusiko julikana .
Aliongeza kuwa katika
upelelezi wa awali wa jeshi hilo linawashikiria watu wawili ambao ni waganga wa
kinyeji Gudawa Yalema (52) msukuma na mkulima wa kijiji hicho.
Alimtaja mtuhumiwa
mwingine kuwa ni Shiwa Masalu (Uselengi) naye mkazi wa kijiji hicho ambaye
alikuwa pamoja na mtuhumiwa wa kwanza wakiwa na vifaa vya kupigia ramli, huku
akieleza chanzo cha tukio hilo ni imani za kishirikina.
Mkubo amewataka wananchi
wenye taarifa juu ya wahusika wa tukio hilo kutoa taarifa hizo kwa jeshi hilo,
ikiwa pamoja na kuwataka kutodanganyika kuwa utajiri unakuja kwa imani za
kishirikina, bali unaletwa kwa kufanya kazi kwa bidii.
Alisema kuna baadhi ya
waganga wanawadanganya wateja wao kuwa viungo vya mlemavu wa ngozi vinaleta
utajiri hali ambayo inawanafanya baadhi ya watu kuamini na kuendeleza mauaji ya
Albino
0 Response to "ALBINO AUWAWA KIKATILI WILAYANI BARIADI"
Post a Comment