Habari za hivi Punde

MGODI WA AFRICAN BARRICK WASHIRIKIANA NA WANANCHI KUBORESHA MAZINGIRA KILA MWAKA HUTENDA KIASI CHA DOLLA KUMI ,MKOA WA SHINYANGA WAUPONGEZA.


Ukongozi wa mkoa aliyefaa suti ya rangi ya maziwa ndio katibu tawala wa mkoa Anselm Tarimo sanjari na mkuu wa wilaya ya Kishapu ambaye alikuwa ni kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga aliyevaa shati la maua wakiwa katika  banda la mgodi wa Bulyanhulu  wakielezwa namna ya ufanyaji kazi za mazingira kwa kushirikiana na jamii ambapo afisa mahusiano mwanadamizi Moses Msofe akiwaeleza kuwa kila mwaka hutenga kiasi cha dolla kumi kwa lengo la kutekeleza miradi mbalimbali  kwa wananchi sanjari na utunzaji wa mazingira.


Afia mazingira  Naziel Eliakimu kutoka Afirican Barrick Buzwagi  akielezea namna ya vifaa mbalimbali wanavyofanyia kazi za utunzaji mazingira.


Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje akikaribisha wageni walioko meza kuu sanjari na utambulisho wa halmashauri hiyo.



Afisa  wa mazingira kutoka mgodi wa Barrick Buzwagi Tunzo Msuya akimueleza kwa ukaribu sana katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Anselmo Tarimo jinsi ya utunzaji mazingira na vifaa wanavyotumia kuepuka na wadudu wabaya pindi wanapo safisha mazingira ikiweo wadudu hatari kama nyoka.


Mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akipokea miche kama ishara ya maadhimisho ya siku ya mazingira duniani kwa upandaji miti pia kutoka kwa afisa  mazingira wa mgodi wa African Barrick Bulyanhulu.


Aliyeshika maiki ni afisa mahusiano mwandamizi wa  mgodi wa Barrick Buzwagi anayefahamika kwa jina la Moses Msofe akielezea uongozi wa mkoa wa Shinyanga namna ya ufanyaji kazi wa utunzaji mazingira.


Afisa mazingira  Tunzo Msuya kutoka mgodi wa Barrick Buzwagi uliopo wilayani Kahama akiwa ameshika miche kwaajili ya kuwagawia wananchi kwaajili ya kupanda kwenye maadhimisho ya  siku ya mazingira.


Mkuu wa wilaya ya Kishapu  Wilson Nkhambaku akipokea cheti baada ya wilaya hiyo kuibuka na ushindi wa utunzaji mazingira kimkoa.


Mkoa wa Shinyanga umeadhimisha siku ya mazingira duniania katika kijiji cha Shilabela kata ya Pandagichiza  halmashauri ya wilaya ya Shinyanga   kimkoa ambapo imeelezwa kuwa   utunzaji wa mazingira umeelezwa kuwa ni changamoto kubwa  wananchi kutozingatia kanunu safi za afya bora kwenye mazingira wanayoishi.
Afisa misitu na Mazingira kutoka halmashauri ya  wilaya hiyo Thadeo Masanja alisema kuwa  kutokana na miti iliyopandwa kwa muda wa miaka mitano ndani ya halmashauri ni  miti 3090 kutokana na hali  ya hewa kuwa kame na kupata wastani wa mvua mm900-600 kwa mwaka husababisha kutostawi vizuri ikiwemo matumizi ya nishati ya kuni  zaidi ambapo asilimia 94 ndio wanaotumia nishati hiyo.lakini bado kunachangamoto  ya ujengaji bora wa vyoo ikiwa asilimia 22.7 wakazi wa halmashauri hiyo hawana vyoo, na zenye vyoo bora ni asilimia 68.3.Naye Afisa mshauri wa mazingira  na mistu Billie Edimott alisema kuwa suala la usafi ni  muhimu ikiwa halmashauri ya wilaya ya Kishapu imeweza kuongoza kimkoa kwa utunzaji wa mazingira,ikifuatiwa na  wilaya ya Kahama  ambapo kijiji cha Fala kiliibuka na ushindi pamoja na shule ya msingi iliyopo wilayani Kahama  hivyo kauli mbiu ya mwaka huu ni TUNZA  MAZINGIRA ILI YAKUTUNZE.
Hata hivyo  mgodi wa African Barrick uliopo Buzwagi na Bulyanhulu waliweza  kuadhimisha  siku hiyo kwa kueleza namna wanavyotunza mazingira kwa kushirikiana na jamii.
Afisa mahusiana  mwandamizi  Moses Msofe alisema kuwa  wamekuwa wakifanya zoezi la upandaji miti  kwa mwaka miche 30,000 hadi 50,000  ikiwa hutenga fedha zaidi ya Dolla millioni 10 kwaajili ya kuendesha  miradi mbalimbali kwenye jamii ikiwemo utunzaji mazingira.


0 Response to "MGODI WA AFRICAN BARRICK WASHIRIKIANA NA WANANCHI KUBORESHA MAZINGIRA KILA MWAKA HUTENDA KIASI CHA DOLLA KUMI ,MKOA WA SHINYANGA WAUPONGEZA."

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.