Habari za hivi Punde

WADAU WA AFYA MKOANI SHINYANGA WAWEKA MIKAKATI YA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WALIOCHINI YA UMRI WA MIAKA MITANO IKIWA VIMEONGEZEKA KUTOKA ASILIMIA 46 MWAKA 2012 HADI KUFIKIA ASILIMIA 61 MWAKA 2013.





Mratibu wa masuala ya ukimwi  katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga Mawazo  Amir Salehe  akiongelea  maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa mama mjauzito kwenda kwa mtoto na watoto wadogo waliokwenye maambukizi  kupata changamoto ya kutopata dawa kutokana na walezi au wazazi  kukosa elimu hiyo na kutofuata ushauri wa kitaalamu wanavoeleza pia.


Sheikh Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ismail  Habib Makusanya  akiwa katika washa  ya wadau wa afya huku akieleza kuwa vifo vya mama na watoto vinatokana na ukosefu wa lishe  na kufanya kazi ngumu pindi anapokuwa amejifungua.


Wadau wa afya wakimsikiliza mganga mkuu wa mkoa Ntuli Kapologwe ambaye hayupo pichani akiwasilisha  mikakati na takwimu za kiwango cha vifo vilivyo fikia ikiwa  mkoa wa shinyanga ulikuwa na asilimia 46 mwaka 2012 na  mwaka 2013 vimeongezeka na kufikia asilimia 61.


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga  akiongoza washa   ya kujadili kupunguza vifo vya wazazi na watoto wachanga  waliochini ya miaka mitano iliyofanyika ndani ya ukumbi wa mkoa na kila halmashauri kuweka mikakati yake ya kupunguza  tatizo hilo  na kuweka maazimio ya utekelezaji ifikapo mwezi Desemba mwaka huu utekelezaji uwe umefanyika. wa kuondoa kabisa.


Mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akielezea  changamoto za afya zinazo wakumba wananchi wa wilaya yake ikiwemo uhaba wa madawa pamoja na damu salama.


0 Response to "WADAU WA AFYA MKOANI SHINYANGA WAWEKA MIKAKATI YA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WALIOCHINI YA UMRI WA MIAKA MITANO IKIWA VIMEONGEZEKA KUTOKA ASILIMIA 46 MWAKA 2012 HADI KUFIKIA ASILIMIA 61 MWAKA 2013."

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.