Habari za hivi Punde

MAADHIMISHO YA SIKU YA SERIKALI ZA MITAA WILAYANI KISHAPU YALIYOFANYIKA KWENYE KIJIJI CHA NEGEZI KATA YA UKENYENGE WILAYANI KISHAPU HUKU WAKIELEZA MAFANIKIO YALIYOPAIKANA KWENYE IDARA MBALIMBALI IKIWEMO KUPATIKANA KWA HOSPITALI YA WILAYA.



Katibu tarafa wa Negezi ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya katibu tawala wa wilaya hiyo ambaye alisimama na kuwakilisha taarifa ya mkuu wa  wailaya hiyo Wilson Nkhambaku  katika maadhimisho ya siku ya serikali za mitaa yaliyofanyika kwenye kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani humo huku akiwaeleza wananchi kuwa bado kunachangamoto ya tatizo la wazazi kuwazuia watoto wao kupata elimu,pia kumekuwepo na changamoto ya ukataji wa miti hovyo bila kupanda sanjari na kukosekana kwa maji hali ambayo ameielezea kuwa hivi karibuni tatizo hilo litakwisha na hivi sasa linashughulikiwa kikamilifu.


Isanga akiwapongeza uongozi mzima wa halmashauri kwa kupata hati safi kwa muda wa miaka miwili mfululizo huku akiwaeleza wananchi waliokusanyika kushuhudia maadhimisho hayo kuwa umoja na mshikamano ndio uliofanya kupata mafanikia halimashauri hiyo,pia aliwapongeza wananchi kulima mazao ya  mtama kwa wingi jambo ambalo limepunguza tatizo la njaa kwenye wilaya hiyo kwa kiasi kikubwa hivyo kilichobaki ni kutafuta maendeleo kwa kasi ambapo katika ni makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Samson Gelewa akiwa sanjari  diwani wa  kata hiyo  Makanasa  Kishiwa.


David Isanga akitoa taarifa kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Wilson Nkhambaku alisema kuwa wazazi wawe na desturi ya kuwasomesha watoto wao kwani ndio tegemeo la taifa la kesho,huku  akisema pia serikali haitasita kumchukulia hatua mzazi yoyote  atakayeshindwa kumsomesha mtoto wake bila kuwepo na sababu za msingi.


Madiwani wa halmashauri ya wilaya  ya kishapu  wakisaini kwenye vitabu mara baada ya kuwasili katika  maadhimisho ya siku ya  serikali za mitaa wilayani humo yaliyofanyika kwenye kijji cha  Negezi kata ya Ukenyenge .


Madiwani wakisikiliza taarifa iliyokuwa ikisomwa na  afisa mipango wa  halmashauri hiyo Fares Mahushi amambaye hayupo pichani.

Madiwani wakiwa katika  moja ya  sehemu waliyokuwa wameandaliwa kuketi katika maadhimisho hayo huku wakiendelea kusaini vitabu mbalimbali  juu ya kuwasili kwao kwenye maadhimisho hayo yaliyofanyika katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu. mkoani Shinyanga.


Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wailaya ya Kishapu Samson Gelewe akiwa na diwani wa kata ya Ukenyenge  Makanasa Kishiwa kwa pamoja  katika meza kuu wakishangilia kwa kupiga makofi mara baada ya  aliyekuwa mgeni rasmi  kueleza kuwa viongozi hao wamekuwa na umoja  na kufanya kazi kwa bidii  ambapo wamefanikiwa kupata hati safi ndani ya halmashauri hiyo kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo.

Viongozi hao walioketi meza kuu walikuwa wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikisomwa na  afisa mipango  Mahushi katika utekelezaji wa  miradi ya maendeleo ikiwemo mafanikio ya  ongezeko la  chakula na utekelezaji kwenye kilimo cha zao la mtama  ,masuala ya elimu  kwa kuongeza vyumba vya madarasa  kutoka 780  mwaka  2006 hadi 1,053 mwaka 2014 upandaji miti  sanjari na utunzaji mazingira.

Makamu mwenyekiti   Samson Gelewe akishukuru  baada ya mgeni rasmi  David Isanga kumaliza kazi ya  kutoa taarifa za kueleza changamoto mbele ya wananchi ambao hawapo pichani.

Kaimu  katibu tawala wa wilaya ya Kishapu ambaye ni afisa tarafa wa  Negezi David Isanga akishiriki kufurahi na diwani wa kata hiyo  Makanada Kishiwa  kwaya ya AIC iliyokuwa ikitumbuiza katika maadhimisho ya siku ya serikali za mitaa.


Mjumbe wa NEC kutoka halmashauri ya  wilaya ya Kishapu  Boniface Butondo akiwasalimia wananchi kwenye maadhimisho ya siku ya serikali za mitaa ambao hawapo pichani.


Afisa mipango wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu  Fares Mahush akisoma taarifa  fupi kuhusu  utekelezaji wa miradi mbalimbali za sekta ya maendeleo  katika maadhimisho ya siku ya serikali za mitaa amapo alisema kuwa  asilimia 88.1 ya wakazi wa   Kishapu wanategemea kilimo  ikiwa zao kuu la biashara  ni zao la pamba  ikiwemo ufugaji wa mifugo ya aina mbalimbali  hivyo halmashauri  imeendelea  kutekeleza  miradi mbalimbali  ya maendeleo  kwa kuzingatia  sera  za kitaifa ,vipaumbele  vya sekta ikiwemo dira ya maendeleo  ya taifa ya mwaka 2025 pia aliyesimama pembeni yake ni afisa habari wa halmashauri hiyo John Mlyambate.


0 Response to "MAADHIMISHO YA SIKU YA SERIKALI ZA MITAA WILAYANI KISHAPU YALIYOFANYIKA KWENYE KIJIJI CHA NEGEZI KATA YA UKENYENGE WILAYANI KISHAPU HUKU WAKIELEZA MAFANIKIO YALIYOPAIKANA KWENYE IDARA MBALIMBALI IKIWEMO KUPATIKANA KWA HOSPITALI YA WILAYA."

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.