Habari za hivi Punde

POLISI SHINYANGA WAKUTANA NA WADAU WA ULINZI NA USALAMA KATIKA SIKU MAALUM YA POLISI MKOA WA SHINYANGA

Hapa ni katika ukumbi wa Karena Hotel mjini Shinyanga  wakati wa (warsha)siku maalum ya polisi mkoa wa Shinyanga( Special Police Day)ambako leo wadau mbalimbali wa ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga wamekutana kujadili namna ya kuimarisha ulinzi na usalama katika mkoa huo.Mgeni rasmi alikuwa naibu meya wa manispaa ya Shinyanga ndugu David Nkulila huku mwezeshaji akiwa ni mkuu wa tathamini na ufuatiliaji wa jeshi la polisi nchini naibu kamishina Mpinga Marco Gyumi 

Mgeni rasmi naibu meya wa manispaa ya Shinyanga ndugu David Nkulila akiwahutubia wadau wa ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga wakati wa siku maalum ya polisi mkoa wa Shinyanga.Nkulila alisema ili kuendelea kuwa na usalama,amani na utulivu nchini ni vyema kukumbushana na kutathmini nini kinahitajika katika kuimarisha ulinzi na usalama hivyo kuboresha utendaji wa jeshi la polisi,wadau na wananchi kwa ujumla.Aidha Nkulila alisema hayo yanawezekana endapo wadau wote kuacha utendaji wa kimazoea na kubadilika kifikra ili kuleta tija


Wadau wa ulinzi na usalama wakiwemo wakiwemo wadau wa ndani ya jeshi la polisi,wazee maarufu,wafanyabiashara,viongozi wa dini na siasa,viongozi wa serikali,waandishi wa habari na wengine wengi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Shinyanga.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Kihenya Kihenya akitoa hotuba ya ufunguzi wa siku maalum ya polisi mkoa wa Shinyanga iliyofanyika katika ukumbi wa Karena Hotel mjini Shinyanga.Pamoja na mambo mengine Kihenya alisema mkoa wa Shinyanga bado unakabiliwa na changamoto ya mauaji ya vikongwe vitendo ambavyo alisema vinatokana na ujinga kwani wanachi wamekuwa wakiamini sana ramli za waganga wa kienyeji matokeo yake wanaua watu wasio na hatia,kitendo ambacho ni kwenda kinyume na sheria za nchi na haki za binadamu.Kamanda Kihenya amemaliza muda wake mkoani Shinyanga na sasa amehamishiwa  Temeke jijini Dar es salaam
Wadau wakimemo waandishi wa habari wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini,Mambo kadha wa kadha yalijadiliwa kama vile utaratibu wa ajira katika jeshi la polisi,ambapo ilielezwa kuwa utaratibu uliopo sasa ni kujaza selform katika taasisi,shule na vyuo husika chini ya usimamizi wa uongozi wa taasisi/shule au chuo husika
Mwezeshaji katika warsha hiyo ,Mkuu wa tathamini na ufuatiliaji wa jeshi la polisi nchini naibu kamishina Mpinga Marco Gyumi akizungumza,ambapo aliwataka wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga na nchi kwa ujumla wenye biashara kubwa zenye mikusanyiko ya watu waagizwe kufunga kamera za CCTV katika maeneo yao ya biashara ili kusaidia kuzuia na  kutanzua mapema  uhalifu unaoeweza kutokea katika maeneo yao ya biashara.Katika hatua nyingine alisema  ili kuimarisha ulinzi katika jamii watu wote wanaohamia katika mitaa wajiorodheshe kwenye daftari la wakazi ili kutambua wakazi husika wa eneo hilo.
Aliyesimama ni Mkuu wa tathamini na ufuatiliaji wa jeshi la polisi nchini naibu kamishina Mpinga Marco Gyumi akizungumza katika warsha hiyo.Alisema jeshi la polisi kwa kushirikiana na wadau na jamii limefanikiwa kuanzisha mkakati wa ulinzi shirikishi/polisi jamii kwa kuwa na miradi/programu ambatano 20 kwa ajili ya kuzuia zaidi,kukabili na kutanzua uhalifu katika himaya mbalimbali ambapo katika mkoa wa Shinyanga umetekeleza kwa ufanisi programu ya usalama wetu kwanza.Shule zilizopata elimu ni Buluba sekondari,Uhuru sekondari pamoja na Jomo Kenyata na Mapinduzi shule ya msingi
Warsha inaendelea-Hivi sasa nchini kuna vikundi 5052 vya ulinzi shirikishi na mkoa wa Shinyanga una vikundi vya ulinzi 150
Mkuu wa upelelezi mkoa wa Shinyanga Hussein Kashindye(aliyemaliza muda wake mkoani Shinyanga) akizungumza katika warsha hiyo ambapo aliwashukuru wadau wote na wananchi kwa ujumla kwa ushirikiano waliompa kwa kipndi cha miaka mitatu na nusu aliyoitumikia Shinyanga na sasa amehamishiwa makao makao jijini Dar es salaam na kuwataka wadau kuendelea kupiga vita suala la mauaji ya vikongwe mkoani Shinyanga ambako kila mara kumekuwa kukiripotiwa mauaji ya vikongwe

Wadau wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini,ambapo ilielezwa kuwa hivi sasa hali ya ulinzi na usalama kwa nchini inakwenda vizuri japo kunakuwa na matukio ya hapa na pale ya uhalifu lakini kwa ushirikiano na wadau werevu na wanajamii kwa ujumla,wahusika wa matukio hayo hubainika na kuweza kuupata mtandao wa uhalifu husika
Mkuu wa upelelezi(mpya) mkoa wa Shinyanga Mussa Athuman Twaibu akizungumza katika siku maalum ya polisi mkoa wa Shinyanga ambaye alisema ili kufikia malengo yanayotakiwa wadau wa ulinzi na usalama wote wanapaswa kushirikiana
Mkuu wa wilaya ya Kishapu ndugu Wilson Nkhambaku akizungumza katika warsha hiyo ambapo alieleza kusikitishwa na vitendo vya uhalifu vinavyoendelea katika jamii ikiwemo mauaji ya vikongwe huku akiongeza kuwa kumekuwepo changamoto ya viongozi wa vitongoji,vijiji,sungusungu kutotoa ushirikiano kwani wakati mwingine matukio yanatokea na viongozi hao wapo na hawatoi taarifa

Katika kuimarisha ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga,kumeanzishwa mikakati mbalimbali kama vile mkakati ulinzi shirikishi/polisi jamii,jeshi la polisi kushiriki katika vikao vya kamati ya ulinzi na usalama vya mita,vijiji na vitongoji,kusogeza huduma za kipolisi hadi katika serikali za mitaa,kuanzishwa kada ya wakaguzi wa polisi wa tarafa/jimbo na kuanzishwa madawati ya jinsia katika vituo vya polisi kwa ajili ya kuelimisha na kuzuia unyanyasaji wa kijinsia na madhila kwa watoto.


Mikakati mingine iliyoanzishwa na jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga katika kupiga vita uhalifu ni pamoja na kuanzishwa kwa madawati ya maadili na malalamiko katika komandi zote za polisi mkoa/vikosi,kuimarisha doria za pikipiki pamoja na kuhamasisha na kuhimiza mamlaka za halmashauri pamoja na wenyeviti wa serikali za vitongoji,mitaa,vijiji na kamati zao za ulinzi na usalama kutekeleza mkakati wa halmashauri wa kuzuia uhalifu pamoja na miji salama sambamba na kuimarisha miundo mbinu ya utendaji kazi kama vile magari kila wilaya

 Baada ya warsha baadhi ya wadau mbalimbali wa ulinzi na usalama wakapata fursa ya kupiga picha ya pamoja na mgeni rasmi pamoja na maafisa mbalimbali wa jeshi la polisi
 Upigaji picha ya pamoja unaendelea,kila mdau alipiga picha 
 Katika warsha(siku maalum ya polisi mkoa wa Shinyanga)mgeni rasmi naibu meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila alisema wahalifu wanaishi katika familia zetu hivyo kwa kushirikisha jamii katika kada mbalimbali ni rahisi kuondoa tatizo au kero za uhalifu/wahalifu kwa kuzingatia mambo mbalimbali kama vile kuwa na uongozi imara katika himaya wenye kujali ushirikishwaji,mahusiano na makubaliano,ushiriki endelevu wa wadau werevu na jamii unaolenga kutatua kero ama matishio ya kiusalama kuanzia ngazi ya familia.Lakini pia alisema kunahitajika uhusiano wa karibu na wa dhati kati ya polisi na jamii pamoja na uhamasishaji katika kujenga na kuimarisha miundo mbinu ya amani na kukubali mabadiliko ndani ya jamii husika.

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog- Shinyanga
KARENY. Powered by Blogger.