Habari za hivi Punde

BAADHI YA WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA MKOANI SIMIYU WAELEZA CHANGAMOTO WALIZOKUMBANA NAZO MSIMU WA KILIMO HUKU MIZANI ZIKIENDELEA KUCHAKACHUA MSIMU WA MAUZO NA HAKUNA UFUMBUZI ULIOPATIKANA DHIDI YA MALALAMIKO YALIYOKUWA YAKITOKEA KILA WAKATI WA MSIMU WA KILIMO CHA ZAO HILO.

Jimmy  Luhende ambaye ni mkurugenzi  wa asasi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na utawala bora vijijini  (ADLG)  ambapo shirika hilo limewezeshwa na  ufadhili kutoka jukwaa la mashirika yanayosimamia  masuala ya kilimo (ANSAF) anasema kuwa  shirika hilo limekuwa na malengo mahususi  ya kuongeza sauti  ya wakulima  kuhusu kilimo  changamoto na kutoa mapendekezo,hivyo  kumekuwepo na  takwimu nyingi ikiwemo changamoto lakini matokeo yake  hakuna majibu Luhende  katika mdahalo huo anasema kuwa  changamoto walizozibaini kutoka kwa wakulima ni sumu ya kupulizia  pamba  ni hafifu tena kuuzwa bila stakabadhi,kilimo cha mkataba  hakikutekelezwa vizuri ambapo wakulima walisema  mkataba  hauja tamka suala la bei,gharama za uzalishaji  kuwa juu tofauti na hali halisi ya mapato kiwemo vijiji vingi  hawajui asilimia 10 ya pamba  kutoka halmashauri kuwa ni shilingi ngapi.

Mtafiti wa kujitegea  Geofrey Chambua anasema kuw   kilimo cha zao la pamba kimekuwa na changamoto nyingi ikiwa hata uzalishaji wake umeonekana kushuka kwa mwaka 2012/13 tani  351,151 na kushuka kwa mwaka 2013/14 tani 246,767.huku akisema kuwa  sera ya kilimo inatakiwa kufanyiwa marekebisho ikiwa inalenga mageuzi  ya sekta  hiyo kwa kuwa  kuongeza tija na uzalishaji wa mazao mbalimbali hivyo inachotakiwa serikali kutekeleza matamkwa yote  ambayo yanaonekana   kutofanyiwa kazi na kumuacha mkulima akinyonywa  kwa kuanzia  upatikanaji wa pembejeo iliyokwisha muda ,mbegu kutoota sanjari na utumiaji wa mizani kuchakachuliwa  hapo uzalishaji utakuwa hakuna tena ndio maana wakulima wamekuwa wakilalamika kila  mwaka msimu unapowadia.

Wadau wa kiimo cha zao la pamba kutoka katika wilaya ya Itilima na Bariadi wakiwa kwenye mdahalo wa kujadili changamoto mbalimbali zinazolikabili zao la pamba mkoa wa Simiyu,ambapo wamezitaka mamlaka zinazohusika na zao hilo kuacha kukaa tu ofisini baadala yake waanze kuwatembelea wakulima vijijini ili kubaini changamoto zilizopo likiwemo suala la bei,mbegu na madawa ya kuuwa wadudu waharibifu.                                                                 Wadau hao pia waliainisha changamoto mbalimbali ambazo zinachangia zao hilo  kuendelea kutokuwa na ubora hivyo kukosa thamani kuwa ni pamoja na baadhi ya wakulima kuweka mchanga,sukari,chumvichumvi na maji ili kuongeza uzito kufidia kilo zinazoibwa kwenye mizani ya pamba. wakati wa kuuza kwa mawakala wa kampuni za kununua zao hilo.


Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi wakiwa katika ukumbi wa Bariadi motel wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa zote zikilenga kupata ufumbuzi wa changamoto za zao la pamba.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wiaya ya Bariadi Bahati Magamula akifungua mdahalo uliowashirikisha wadau wa zao hilo,wakulima ,wataalamu wa kilimo kutoka halmashauri na waandishi wa habari,mdahalo ambao umeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na demokrasia na utawala bora vijijini (ADLG) chini ya ufadhili wa jukwaa la mashirika yanayojishughulisha na kilimo ANSAF.
Mkulima wa zao la pamba kutoka kijiji cha Mwamapalala wilaya ya Itilima Kalibashia Jilinde akieleza hasara aliyoipata kutokana na kutumia mbegu za pamba za Quiton ambazo hazikuota na kulazimika kurudia mara tatu lakini pia hakufanikiwa,ameitaka serikali  kufanya utafiti wa kina kujua madhara na faida zake  kabla ya kupeleka kwa wakuima kwani wamechangia kuwadidimiza kiuchumi kutokana na kutumia gharama kubwa bila kupata faida.
Wakulima wa zao la pamba wakifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa na wawezeshaji katika kupata mbinu mpya , maoni,ushauri na mapendekezo ya kuondoa changamoto zilizopo.
Mdahalo bado unaendelea
Katibu wa mtandao wa vikundi vya wakulima (MVIWATA) wilaya ya Bariadi Zabron Sayi akiwaasa wakulima wenzake kutoacha kuendelea kulima kilimo cha pamba na aliitaka serikali kupitia wizara husika kuhakikiha inawachukulia hatua watumishi wa ngazi za chini wa idara ya kilimo kutokana na kuwepo uzembe mkubwa wa kutowatembelea wakulima ili kufahamu kero mbalimbali zinazo wakabili badala ya kwenda kukamata wakulima walichanganya pamba na mazao mengine.
Wadau wakiwa kwenye ukumbi wa Bariadi motel kwa ajili ya mdahalo wa kujadili changamoto mbalimbali za zao la pamba ikiwa ni pamoja na bei kuendelea kuwa chini ambayo haina tija kwa mkulima.
Mkulima wa pamba kutoka kijiji cha Mlimani kata ya Zagayu Sele Mayenga ambaye alisema ameamua kuachana na kilimo cha pamba kwa kuwa haoni faida kutokana  na kupanda mbegu za Quiton na kushindwa kuota hivyo kuamua kujikita katika kilimo cha mahindi na alizeti.


Wadau wa kilimo  cha pamba mkoa wa Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja.
KARENY. Powered by Blogger.