Habari za hivi Punde

MFUKO WA VYOMBO VYA HABARI (TMF) WAKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI MKOANI SHINYANGA LENGO KUWASILISHA MAWAZO YAO.


Mwandishi wa  habari mkongwe Ndimara  Tengambwage  akiwasikiliza waandishi wa habari mkoani Shinyanga ambao hawapo pichani  mara baada ya kutembelewa na  viongozi wa mfuko wa vyombo vya habari nchini (TMF)  huku waandishi wa habari wakielezwa kuwa wanawajibu wa kutumia mfuko huo katika utendaji wao wa kazi hasa kwenye maeneo ya vijijini au changamoto yoyote kuibua kwa lengo la kufahamika ili wenye wajibu waitekeleze,ambapo pia walielezwa kuwa waandishi wa mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa waandishi ambao hawajawahi kuomba  kupitia mfuko huo isipokuwa waandishi wawili hivyo wametakiwa kutumia fursa hiyo kwa kwenda na mawazo yao na kuyawasilisha ili kuona wazo gani linaloweza kufaa na kufanyiwa kazi.


Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakiwa katika semina iliyoandaliwa na mfuko wa vyombo vya habari (TMF) iliyofanyika  ukumbi wa mwalimu house.


Miongoni mwa waandishi  wakongwe mkoani Shinyanga ni bi Moshi Ndugulile ambaye anasoma gazeti yeye ni  mtangazaji na mwandishi wa redio Faraja huku aliyevaa miwani   na suti nyeusi ni mwandishi mkongwe Anthony  Komanya wa magazeti ya uhuru na mzalendo.


Waandishi wa habari wakisikiliza kwa umakini mkubwa  namna ya kuandika wazo.


Bi Edda Sanga na Ndimara  wakiwa meza kuu ambao wamepewa jukumu  na uongozi wa TMF kuwa majaji wa kusikiliza mawazo ya kila mwandishi aliyehudhulia semina hiyo.


Mwenyekiti Shija Felician akiwa na mwadishi wa gazeti la jamboleo Stephen Kidoyai kwenye semina ya TMF


Edda Sanga akiwa anajiandaa kusikiliza mawazo kutoka kwa waandishi wa habari  wanaoripotia redio.


Mwandishi wa habari ambaye pia ni reporter wa redio Faraja iliyopo  mjini Shinyanga  Veronica  Natalis  Mataba  akiwasilisha wazo lake kwa  Edda Sanga ambaye alipewa jukumu la kupitia mawazo kwa  waandishi wa redioni pekee.


Japhet Sanga  ambaye ni  afisa ruzuku  wa TMF akiwaeleza waandishi wa habari  ambao hawapo pichani kwanini wamekuwa hawaombi fedha kutoka kwenye mfuko huo ikiwa mkoa huo unachangamoto mbalimbali zinazotakiwa kujulikana na wananchi ikiwemo serikali na kuzifanyia kazi hivyo aliwataka waandike maombi ya wazo walilo nalo litaangaliwa na kupokelewa kama linaweza kuleta mabadiliko katika jamii.


Tengambwage akiwaeleza waandishi wa habari namna ya kuchanganua  wazo ili kuweza kulifanyia kazi na wazo hilo linaweza kuibua maswali mengi  ambayo ndio yanatakiwa kufanyiwa kazi na kuleta mabadiliko.

KARENY. Powered by Blogger.