Habari za hivi Punde

MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA KISHAPU WAMEIOMBA SERIKALI KUWALIPA FIDIA HARAKA WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA WALIOPATA HASARA.


MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KISHAPU MKOANI SHINYANGA JUSTINE SHEKA AKIAHIRISHA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI.

MADIWANI wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga  wameitaka  wizara ya  kilimo,chakula na ushirika  kuhakikisha wanawalipa fidia wakulima wa zao la pamba kwani hivi sasa wanateseka kwa kukosa fedha na chakula  huku  wakishindwa kuendesha maisha yao,  ikiwa zaidi walikuwa wakitegemea zao hilo kujinyanyua kimapato ndani ya familia.

Sio kwa wakulima pekee hata halmashauri  zitapata hasara  ikiwa  tayari vibali vimekwisha tolewa kutoka bodi  ya pamba  kwa wafanyabishara  wa zao la pamba   huku wengine wakidaiwa kwenye msimu uliopita  kwa makubaliano yalivyokuwa  mpaka wakiuza ndipo halmashauri inakata pesa , leo hii zimesitishwa kuchukua ushuru  kuna wasiwasi kutorejesha fedha  hizo wafanyabishara kwenye halmashauri.

 Hayo waliyasema   kwenye kikao cha baraza la madiwani  liliofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo  ambapo  walimtaka mkurugenzi  Jane  Mwitagurwa  kuandika barua kwenda  kwa waziri mwenye dhamana  kuhakikisha fedha hizo zinalipwa ikiwa tathimini kwa wakulima  tayari huku uthibitisho wa mbegu zilizotolewa na mkuu wa wilaya pamoja na mkuu wa mkoa upo mbegu hazikuota.

Diwani wa kata ya Sekebugoro  Ferdnand  Mpogomy alisema kuwa   vibali vya  ushuru wa pamba vimetolewa na bodi kwa wafanyabishara ikiwa wengine ni wadaiwa wamepewa vibali hivyo sasa hoja iliyopo halmashauri imezuwiwa kudai ushuru,  fedha  zinazodai wafanyabishara hao  itakuwaje? Waliitaka bodi ya pamba kujibu namna  ya  upatikanaji wake  ili ziweze kurejeshwa halmashauri.

“Sasa pamba imekosa thamani ni bora wakulima walime mazao mengine na kuachana na zao hilo, hakika nawaeleza mwakani watalima wachache mwaka unaofuata hakuna atakaye lima kwani wakulima wameteseka vyakutosha  walikuwa wanalitegemea kujinyanyua kimapato ndani ya familia sasa imekuwa kilio hakuna msaada kinachotakiwa wizara ituhakikishie ni lini  wakulima watalipwa fidia ya gharama walizotumia?”alisema  diwani Mpogomy.

Diwani kutoka kata ya Mondo John Ndama alisema  kuwa katika vikao walivyokaa  walidai kuwa  fedha hizo zitalipwa  ikiwemo wakulima kwani   wameathirika tangu mwaka jana mwezi Novemba  na tahimini imeshafanyika walipwe haraka, pia diwani wa kata ya  Songwa Mohamed Shabani alisema kuwa  maongezi na bodi ya pamba  hawataki kwani ndiye aliyesababisha  hali kuwa mbaya kwa wakulima kutangaza mbegu zisizoota ikiwemo madawa feki.

“Mimi kwenye vijiji vya kata yangu wapo watu wa bodi ya pamba  ambao wamekuja kusimamia ,hakuna  faida ya kuwepo kwani  wameleta uongo kwenye matumizi ya mbegu zisizo na manyoya , pia inashangazwa wizara kuendelea kuwakumbatia  huku ikiwapa jukumu la ukusanyaji ushuru kama walishindwa kuleta mbegu bora na madawa sasa kwenye ukusanyaji  ushuru ndio wataweza au ndio wataiingizia hasara serikali”alisema diwani wa kata ya Songwa  Mohamedi.

Naye mwenyekiti wa halmashauri hiyo Justine   Sheka  alisema kuwa  wanaiomba serikali kupitia bodi ya pamba  kuhakikisha  wanawajali wakulima  kwani madiwani wanauwezo  wa kuwahamasisha wakulima wa zao la pamba kuacha  kulilima kabisa na kufuata mazao mengine kutokana na hasara waliyoipata  mbegu kutoota.

 “ Tatizo la  mbegu kutoota lilikuwa ni kubwa  katika  halmashauri hii wakulima zaidi ya 13OO mashamba yao hayakuota na hivyo kupata hasara ya zaidi ya billion 1.6.  hiyo yote imetokana  na wanasiasa kudharauliwa   na kupuuzwa lakini wangefutilia tangu mwanzo hasara hii ingekuwa kidogo au isingekuwepo”alisema Sheka.

Kwa upande wake mkaguzi kutoka bodi ya pamba wilaya ya Kishapu  Thomas  Tiluhongelwo  alisema kuwa  halmashauri zinahusishwa  kupitia  kwenye vijiji kufanya tathimini,kuhusu madawa  ya kuua wadudu bod haihusiki, ila kuhusiana na mbegu mwaka huu watajitahidi  ziwe na ubora  pia  kabla ya kufikia msimu wa kilimo kuanza  wizara imesema itahakikisha  wakulima wote waliopata hasara  wawe wamelipwa.
KARENY. Powered by Blogger.