Habari za hivi Punde

BAADHI YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI HALMASHAURI YA MASWA WAGOMA KUCHANGIA FEDHA KWAAJILI YA MBIO MWENGE WA UHURU


NAIBU WAZIRI WA ELIMU  NA MAFUNZO YA UFUNDI   Philipo Mulugo.

BAADHI ya Walimu wa Shule za Msingi katika wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu wamepinga mchango wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa madai kuwa mchango huo ni miongoni mwa michango ya hiari na siyo ya kulazimishwa wala kutishwa kwa wale ambao hawatachanga mchango huo huku wakidai mshahara wanaoupata ni kidogo.


Wakiongea na waandishi wa habari  walimu hao walisema kuwa Waratibu wa Elimu Kata na Walimu  Wakuu wanawalazimisha kuchanga mchango huo ambao wanadai kuwa hawaoni faida yake.

Huku wakikosoa mbio za mwenge  wa Uhuru na kutaka ufutwe kwa maelezo kuwa hauna tija kwa sasa, ambapo baadhi yao wakibainisha kuwa hawako tiyari kutoa michango huyo kutokana na mishahara yao kuwa kidogo.

“siko tiyari mimi kutoa mchango wangu..kwanza mshahara wangu ni mdogo..hapa nilipo nina ndugu na wazazi wangu wananitegemea kwa huo mshahara..leo hii unataka nichangie kitu ambachio sioni faida yake..badala yake kina kula hela zetu…kwanza wanilipea madeni yangu..ndipo nitatoa michango” Alisema mmoja wa walimu hao.

Walisema kuwa kama Serikali  inaona thamani ya pesa ya Mwalimu basi ingemwongezea mshahara unaokidhi mahitaji yake sio kama ilivyo sasa ambapo kiwango wanacholipwa ni mateso na ambacho wanalazimishwa kuchangia katika mwenge huo.

Wakionyesha barua ya mchango huo iliyotoka katika Ofisi ya Mkurugenzi  wa Halmashauri ya wilaya ya Maswa kupitia Idara ya Elimu iliwaandikia barua Waratibu Elimu Kata  yenye KUMB Na MDC/ADM.10/VO1 1V.105 ya  Julai 11 mwaka huu ikiagiza kuchangia Mbio za Mwenge huku ikiwa imeanisha viwango .

Viwango hivyo kwa mujibu wa barua hiyo iliyosainiwa na Ofisa Elimu Msingi wilaya ya Maswa,Bujimu Mabeyo inaonyesha kuwa kila mmoja na fedha zao kwenye mabano  Wakuu wa Idara( shilingi  10,000/=),Waratibu Elimu Kata (sh 5000/=),Shule (sh 10,000/=),Mwalimu (sh 2000/=) na CWT
(sh 150,000/=)  pia ikasisitiza Waratibu Elimu Kata wapeleke michango hiyo  Julai 31 mwaka huu.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Maswa,Trasias Kagenzi akizungumzia suala hilo alisema kuwa mchango huo ni moja ya maafikiano yaliyofikiwa katika kikao ambacho hata Chama Cha Walimu(CWT) waliridhia huku akisisitiza ni wa hiari na wala hakuna haja ya kushurutishana kwa kuzingatia kuwa imekuwepo kila mwaka .


 
KARENY. Powered by Blogger.