MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) MKOANI SIMIYU TITUS KAMANI. |
WENYEVITI wa Vitongoji katika kata ya Marambo
Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu wamekitaka chama cha mapinduzi
(CCM) pamoja na serikali kumwajibisha Diwani wa kata hiyo Clementi Matogoro (CCM)
kwa madai ya kutumia ubabe katika kuendesha shughuli za kata hiyo.
Mbali na hilo wenyeviti hao
wametangaza mgomo wa kutokufanya kazi yeyote ya maendeleo ndani ya kata hiyo,
ikiwa pamoja na kutokushiriki katika vikao vya maendeleo vya kata (WDCs), ambapo
katika kikao cha maendeleo cha kata kilichofanyika juzi wenyeviti hao walisusia
kikao hicho.
Wakiongea na waandishi wa habari
katika ofisi za chama cha waandishi wa habari mkoani hapa mara baada ya kususia
kikao hicho, walisema kuwa hawako tiyari kufanya kazi na diwani huyo kutokana
na kuwatukana pamoja na kuendesha kata kwa ubabe.
Walisema kuwa mbali na ubabe pamoja
na kutukanmwa walimtuhumu diwani huyo kuwa chanzo cha wafanyakazi wa serikali
ndani ya kata hiyo kufukuzwa kazi, na kuamishwa pindi wanapopinga maamuzi yake.
Walibainisha kuwa Matogoro amekuwa
akiongea uongo kwa wakuu wa idara katika halmashauri ya mji ili wafanyakazi hao
wafukuzwe kazi au kuamishwa ndani ya kata yake, ambapo waliodai alisababisha
mtendaji wa kata pamoja na mwalimu mkuu shule ya msingi Bariadi kuamishwa na
kushushwa cheo.
“Tulikaa kikao cha maendeleo ya kata
tarehe 16/04/2014..tukakubalina kuuza miti kwa wananchi wetu ambayo ilkuwa
imekauka katika pori la marambo..tulipomaliza kikao sisi tulienda kuuza miti
hiyo..cha kushangaza..diwani alitugeuka na kuwakamata wananchi wote ambao
tulikuwa tumewauzia miti hiyo” Alisema John Masunga Mmoja wa wenyeviti hao.
Walisema kuwa mbali na wananchi hao
kukamatwa na kupelekwa kituo cha polisi wilaya diwani huyo aliwatuhumu viongozi
hao kuwa ni wezi kwa kuuza miti hiyo kwa maslai yao binafsi jambo walilosema
kuwa uongo.
Alipotafutwa na waandishi wa habari
kwa njia ya simu yake ya kiganjani diwani huyo alikataa kuongelea jambo hilo .
0 Response to " WENYEVITI NA VITONGOJI WILAYA YA BARIADI MKOANI SIMIYU WAMEKITAKA CHAMA CHA MAPINDUZI KUMWAJIBISHA DIWANI AMBAYE CHANZO CHA MGOGORO "
Post a Comment