WADAU WA AFYA WAKIHAMASISHA KUFUATA UZAZI WA MPANGO MKOANI SHINYANGA.
BAADHI ya wazazi na
walezi mkoani Shinyanga wamekuwa wakiwafanyia unyasaji wa kijinsia
watoto wa kike kwa kuwaoza mapema kabla ya umri wao na viungo kutokukomaa
vizuri kwa lengo la kutaka utajiri wa haraka hali ambayo imeonyesha
kuongezeka kwa mimba za utotoni na kufikia asilimia 59 ambapo imeonekana
pia kushindwa kutumia njia ya mpango wa uzazi.
Licha ya mimba za utotoni pia
kumekuwepo na changamoto ya kutopanga uzazi hali ambayo imeelezwa kuwa kwa
mkoa wa Shinyanga uko nyuma kwa wanaotumia uzazi wa mpango ni asilimia 12.5
huku vifo vitokanavyo na uzazi ni asilimia 80 sababu ikielezwa ni mama
mjamzito kuchelewa kufika katika kituo cha afya na wasichana kuzaa umri mdogo.
Hayo yalisemwa na mganga
mkuu wa mkoa dkt Ntuli Kapologwe kwenye ufunguzi wa
semina ya uzazi wa mpango kwa waandishi wa habari wa kanda ya Ziwa na magharibi
kwa mikoa ya Simiyu,Tabora Mwanza, Kigoma ,Geita,Kagera ,Mara na
Shinyanga yaliyofanyika mjini Shinyanga huku akisema kuwa
kufikia mwakani inatakiwa kutimiza malengo ya asilimia 60 na sasa ni
asilimia 27 kitaifa.
“Vifo bado vipo vingi sauti za
waandishi wa habari zikitumika zinaweza kupunguza changamoto iliyopo
kwani afya ya mama na mtoto bado iko nyuma sababu ya
kushindwa kupanga uzazi na kufikia asilimia 12.5 kwa mkoa wa
Shinyanga isipokuwa kwa suala la mtoto pekee limefanikiwa vizuri ambapo
jamii bado inawanyanyasa watoto wa kike kwa kuwaozesha mapema na kufanya ongezeko
la mimba za utotoni huku viungo vyao vikiwa bado kukomaa.”alisema
Dkt Kapologwe.
Mwezeshaji Anna Mwalongo
kutoka mkoani Shinyanga alisema kuwa kuhusu masuala ya mpango wa uzazi
ni muhimu kuwapatia waandishi wa habari semina hii ili waweze kuripoti na
kuleta mabadiliko chanya ikiwa zaidi ya wanawake 8500 kitaifa
hufariki dunia kwa matatizo yanayohusiana na uzazi.
Mwalongo alisema kuwa
ongezeko la watumiaji wa uzazi wa mpango ni asilimia 2.9 kila mwaka
ikiwa wanawake 454 kati ya 100,000 hufariki kwa mwaka, na
kati ya watoto 1000 watoto 51 wanafariki pia, kwa wanaotumia uzazi
wa mpango kwa njia zote ni asilimia 34 huku aslimia 7 wakitumia njia za asili pekee
kupanga uzazi.
“Baadhi ya wanawake wamekuwa
wakinunua dawa za mpango wa uzazi kwenye maduka ya dawa ya watu
binafsi,wasichana wenye umri wa uwezekano wa kupata mimba nao
huwaibia wazazi wa o majumbani hivyo takwimu zake zinashindwa kuhesabiwa
kutokana na wenye maduka kutoorodhesha idadi,pia kutofahamu ni wasichana
wangapi wanatumia,ambapo asilimia 9.5 ya wanawake wanajikuta wakipata
watoto pasipo kutarajia wao huku wakilenga kupanga uzazi”alisema Mwalongo.
Naye mwakilishi kutoka wizara ya
afya na ustawi wa jamii kitengo cha afya ya uzazi na mtoto Zuhura Mbuguni
alisema kuwa kuna baadhi ya vikwazo ambavyo mwanaume
kutomruhusu mke wake kutumia uzazi wa mpango ikiwemo kuishi mbali
na vituo vya afya huku akisema suala la mpango wa uzazi sio kwa wanawake pekee
ni mke na mume au wapenzi.
Vikwazo vilivopo mke na mume au
wenza kutojadiliana kuhusu idadi ya watoto wala kupanga uzazi, wanawake kunyimwa
uwezo wa kufanya maamuzi kuhusu ngono,mimba na matumizi ya uzazi wa
mpango,ukatili wa kijinsia pamoja na ukeketaji huweza kuathiri utoaji
huduma na matumizi ya njia za uzazi wa mpango huku vijana walioanza
kubalehe wanakuwa na hofu kuonwa na watu wakifuata huduma ya uzazi
wampango”alisema Mwalongo.
|
0 Response to " UZAZI WA MPANGO MKOANI SHINYANGA WANAOTUMIA NI ASILIMIA 12.5 BADO KUNA CHANGAMOTO KUBWA"
Post a Comment