Habari za hivi Punde

SHEIKHE WA MKOA WA SHINYANGA AWAASA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU

Waumini wa dini ya kiislamu wakiwa uwanja wa CCM Kambarage  ikiwa ni siku ya Idd el-fitri.

Sherkhe wa mkoa wa Shinyanga Ismail Habib Makusanya akizungumza na waumini wa dini ya kiislamu mara baada ya kumaliza kuswali swala ya Idd el- fitri,ambapo aliwataka kuendelea kuiombea nchi ili amani iliyopo iendelee kuwepo sanjari na mchakato wa kupata katiba mpya umalizike kwa amani na kuwepo maelewano kwa wajumbe wa bunge maalumu la katiba.                                                                                                                                                   
Alisema wakati sasa umefika  kwa  waumini  wa dini hiyo na watanzania wote kuwaombea wajumbe wa bunge maalumu la katiba ili waipitishe kwa amani na utulivu  ,kwani  kumekuwepo na manung’uniko ya kutotendewa haki kwenye  katiba ya sasa na kwamba katiba itakayo kuja itapambanua  haki za kila kiumbe.
“ Katiba hii haitapatika nje ya utaratibu uliopangwa  ila kwa kupitia  sheria na kanuni zilizowekwa,
rai yangu kwenu ninawaasa kutokubaliana na nyumba za ibada zinazoanzisha vurugu na kauli zenye  misigano isiyo na tija katika taifa letu na kauli   zile zisizo watii viongozi wa kitaifa waliochaguliwa kwa kutumikia taifa hili”alisema Sherkhe Makusanya.
 Waislamu wakiwa katika uwanja wa CCM Kambarage
                
Sherkhe Sudy Suleiman akitoa wito  kwa waislamu wote kujibidisha katika  elimu hasa kwa watoto ,ambapo alisema ukitaka kuishi salama katika  dunia na ahera  lazima usome kama alivyohusiwa na  mtume   Mohamad  S.W.A na mwenyezi mungu.
Hata hivyo Sheikhe huyo aliwataka waumini kufuata  mienendo mizuri kama walivyo fanya wakati  kipindi cha mfungo wa mwezi  mtukufu wa Ramadhani  na sio  kufanya matendo maovu ambayo yatamchukiza mwenyezi mungu na kuondoa amani katika familia na taifa kwa ujumla

Waumini wa dini ya kiislamu wakitoka katika uwanja wa CCM Kambarage baada ya kuswali swala ya Idd el fitri.
Sherkhe wa mkoa wa Shinyanga Ismail Habib Makusanya akizungumza na waumini wa kiislamu katika uwanja wa CCM Kambarage.
Trafiki wakiangalia usalama wa rai katika kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri.
Waumini wa dini ya kiislamu wakiwa uwanja wa CCM Kambarage  ikiwa ni siku ya Idd el-fitri.
                                        

0 Response to "SHEIKHE WA MKOA WA SHINYANGA AWAASA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.