Habari za hivi Punde

MAJERUHI WANAOTIBIWA KATIKA HOSPITALI YA MKOA WAPATIWA MSAADA.



BAADHI YA WAFANYAKAZI WA BENKI YA NMB WAKIWA KATIKA WODI YA  WATU WALIOPATA MAJERAHA KATIKA AJALI NA KULAZWA HOSPITALI YA MKOA WA SHINYANGA.
Wafanyakazi wa Banki ya NMB tawi la Manonga manspaa ya Shinyanga wametoa msaada wa vitendea kazi kwenye Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga kufuatia ajali mbili mfululizo ambazo zimesababisha vifo vya watu 3 na wengine kujeruhiwa vibaya.

 Meneja wa benki hiyo James Poneka alisema wafanyakazi wameguswa na matukio hayo ya ajali na kufikia hatua ya kuchanga fedha kwa ajili ya kununua vifaa ambavyo vitasaidia kuokoa maisha ya wahanga wa ajali hizo.

Kwa upande wake mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo dkt  Fredrick  Mlekwa amewapongeza wafanyakazi wa Banki ya NMB kwa kuguswa na matukio hayo ya ajali na kueleza  kuwa   msaada huo umefika kwa wakati ikiwa majeruhi wengine bado wanaendelea kupatiwa matibabu.

Meneja wa benki  tawi la NMB akikabidhi  vifaa tiba kwa mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa  dkt  Fredrick  Mlekwa.
Dkt   Fredrick   Mlekwa   akikagua    baadhi ya vifaa  vilivyotolewa na benki ya  NMB  tawi la Shinyanga  

Wafanyakazi wa benki ya NMB wakiwa na wauguzi katika wodi ya watu wanaopata ajali   kwenye hospitali ya mkoa wa Shinyanga    kulia ni ofisa wa mikopo kutoka benki hiyo   Scholastical  Hyera akiwa na meneja biashara wa    Rudence
    MGANGA MFAWIDHI DR MLEKWA AKITOA MAELEZO JUU YA MAJERUHI WA AJALI YA FUSO KWA MENEJA WA BANKI YA NMB  

BAADHI YA MAJERUHI WA AJARI YA FUSO WAKIPATIWA MATIBABU


0 Response to "MAJERUHI WANAOTIBIWA KATIKA HOSPITALI YA MKOA WAPATIWA MSAADA."

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.