HII NI SHULE YA MSINGI MASAGALA ILIYOPO HALMASHAURI YA WILAYA YA KISHAPU NI KATI YA SHULE KUMI BORA ZILIZOFANYA VIZURI WILAYANI HUMO.
HALMASHAURI ya wilaya
Kishapu mkoani Shinyanga imeweka mikakati ya kuboresha elimu ya shule za msingi kwa kuziondoa changamoto mbalimbali
zinazowakabili ikiwemo kukarabati maboma
ya vyumba vya madarasa, kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la saba huku shule ya kwanza ikizawadiwa
shilingi laki tatu na inayoshika mkia hupewa kinyago.
Hata hivyo kimkoa
katika ufaulu wa shule za msingi ni asilimia
84 kwa upande wa darasa la saba mwaka jana kwenye halmashauri hiyo ikiwa imeshika nafasi ya pili, pia kuna shule za msingi 114 tayari wamepokea walimu 142 kwa mwaka huu ambapo mahitaji ya walimu wa shule za msingi wilaya nzima ni 1639.
Hayo yalisemwa kwenye
baraza la madiwani la halmashauri
hiyo hivi karibuni huku baadhi ya madiwani wakielezea changamoto
ya elimu shule za msingi kuwa uhaba wa
madawati ,maboma mengi yamejengwa bila kukukamilishwa ukiwepo udangangayifu kwenye mitihani pia waelekeze katika shule kumi zilizofanya
vibaya chanzo chake ni nini hasa.
Diwani wa kata ya
Sekebugoro Fernand Mpogomi
alisema kuwa maboma yamekuwepo
mengi yameshindwa kukamilishwa walimu
wana upungufu wa nyumba, uhaba wa madawati
sasa ni suala la kuelekeza kwenye elimu zaidi na kutekeleza hayo mfano shule ya msingi
Mwigumbi imeingia kwenye shule kumi ambazo zimefanya vibaya nini tatizo ikiwa ina walimu wa kutosha na
wanapata chakula cha mchana.
Diwani wa kata ya
Bubiki Boniface Mataba alisema
kuwa tatizo lingine kumekuwepo na michango
mingi masuleni ambayo haina
tija,wanafunzi wanapotoa fedha hawapewi stakabadhi wakati mwingi hupewa lakini hazionyeshi ni
mchango kwaajili ya nini,kama ni suala la maji ,mlinzi au ada basi ziandikwe na
kuonekana kwa kutofanya hivyo wazazi
wanaona huo ni utapeli.
“Michango mashuleni ni mingi haina tija kwani hatuoni
inafanya kazi gani,hata wakitoa wanafunzi hawapewi stakabadhi za malipo wakati
mwingine haziandikwi kuwa ni malipo ya ada au kitu gani, sio kwamba tunaikataa michango ila ionyeshe imefanya shughuli gani ndani ya shule husika”alisema
diwani Mataba.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Justine Sheka alisema
kuwa changamoto zilizopo zifanyiwe kazi
kwa kuboresha miundombinu katika shule hasa kwenye maeneo yanayoelezwa kuwa ni
tatizo,ikiwa kiasi cha shilingi laki
tatu hutolewa kwa shule inayofanya vizuri
na kinyango kwa shule inayokuwa
ya mwisho.
Ofisa elimu wa shule za msingi katika halmashauri hiyo Sostenece
Mbwilo alisema kuwa kimkoa wilaya
hiyo kwenye ufaulu imekuwa nafasi ya pili kwa kupata asilimia 84,ikiwa
changamoto ilionekana katika usimamizi wa mitihani ya moko kuwepo udanganyifu tofauti mitihani wa taifa unavyokuwa makini katika usimamizi wake.
Sostenece alisema kuwa
pia kumekuwepo na shule kumi bora ambazo zimefanya vizuri ikiwemo shule ya msingi Mwadui A na
Masagala ambapo alizielezea kuwa hazina changamoto kama shule zingine za uhaba wa madawati, walimu wa kutosha
walioendana uwiano na wanafunzi ukiwemo ukaguzi wa mara kwa mara na utolewaji wa motisha kwa walimu wa masomo
yaliyofanya vizuri.
Pia shule zilizofanya vibaya
zimelezwa kuwa na changamoto ya
mrundikano wa wanafunzi usioendana na
uwiano wa walimu, uhaba wa madawati , nyumba za walimu ikiwemo ofisi ambapo masuala hayo yote yanachangia kushuka kwa elimu hata ufaulu kwa wanafunzi hao.
|
0 Response to "HALMASHAURI YA WILAYA YA KISHAPU IMEWEKA MIKAKATI YA KUNYANYUA ELIMU."
Post a Comment