SHULE ya sekondari Mwadui iliyopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga inayomilikiwa na kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, imeweka mikakati ya kufukuza wanafunzi wasio waadilifu, wanaovaa sketi futi, milegezo,kuwa na Simu pamoja na kutumia vipondozi wakiwa shuleni hapo.
Hayo yalisemwa na mwalimu mkuu wa Shule hiyo mchungaji Yohana Nzelu kwenye kikao cha bodi ya shule na wazazi mara baada ya kufungua na kuweka jiwe la msingi kwenye bweni jipya la wavulana na kuwa somea wazazi na walezi hao taarifa ya shule pamoja na mipango mikakati ya kuboresha taaluma kwa wanafunzi.
Mwalimu Nzelu alisema moja ya mafanikio kwa wanafunzi katika kufaulu vizuri ni lazima kwanza wawe na nidhamu ya kutosha na maadili mema ambapo bodi hiyo ya shule ilikaa na kujadili namna ya kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wake na kuweka mikakati hiyo ambayo itaondoa wanafunzi kujiingiza katika makundi mabaya.
‘’Shule hii katika matokea ya kidato cha nne mwaka 2012 wanafunzi waliofanya mtihani 61 waliopata daraja la kwanza mpaka la tatu ni wananfunzi wawili na alichaguliwa mwanafunzi mmoja kwenda kidato cha tano”
‘’mwaka jana (2013) wanafunzi 76 walifanya mtihani wa kidato cha nne waliopata daraja la kwanza mpaka tatu 33, waliochaguliwa na serikali kujiunga kidato cha tano wanafunzi 24, na waliokwenda shule binafsi walikuwa Saba ambapo tumepiga hatua, hivyo mikakati iliyopo ni kusisitiza maadili na kuondoa changamoto zilizokuwepo wanafunzi kukosa nidhamu “alieleza walimu Nzelu.
Akizungumza kwenye kikao hicho Askofu mkuu wa kanisa hilo (KKKT) wa dayosisi hiyo Emmanuel Makala ambaye ndiye msimamizi wa Shule hiyo alisema suala hilo si la kupuuzwa na hawatakuwa na msamaha kwa mwanafuzi atakaye kiuka sheria hizo huku akitoa wito kwa wazazi na walezi kushirikiana kwa pamoja.
Askofu makala alisema wazazi na walezi wakishirikana ipasavyo , pamoja na kufuatilia taarifa za watoto wao shuleni itasaidia kwa kiwango kikubwa kuongeza taaluma ya wanafunzi na kupata ufaulu mzuri sambamba na kuzalisha taifa la wataalamu na viongozi wenye maadili.
Askofu huyo pia alifungua na kuweka jiwe la msingi katika bweni Jipya la wavulana katika shule hiyo ambalo limejengwa kwa kugharimu jumla ya Shilingi milioni thelathini na tisa (39,000,000).
Baadhi ya wazazi Japheti Daudi na Stanley Jimbo walisema kuwa hayo yaliyoelezwa wamekubaliana nayo ikiwa uongozi wa Shule hiyo kwa mikakati walioiweka inaweza kufanikisha maadili memahuku wakiahidi kutoa ushirikiano ambapo shule hiyo inajumla ya wanafunzi 282 kidato cha kwanza hadi cha nne wasichana 148 ,Wavulana 134.
|
0 Response to "MCHUNGAJI YOHANA NZELU WA KANISA LA KKKT AWAPASOMO LA MAADILI WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MWADUI."
Post a Comment