Habari za hivi Punde

WANANCHI WA KIJIJI CHA BULEKELA KATA YA MASANGA WILAYANI KISHAPU MKOANI SHINYANGA WAMEKATAA MRADI WA MAJI WA VISIMA VYA KUPAMBU KWA MKONO WAKITAKA KUSAMBAZWA KWA MABOMBA KARIBU NA MAJUMBANI MWAO,MADIWANI WATOA AZIMIO MRADI HUO UHAMISHWE KIJIJINI HAPO NA KUPELEKWA SEHEMU NYINGINE.


HIKI NI KISIMA KIREFU CHA MAJI AMBACHO WANANCHI WAKE HUPATA   MAJI HAYO KWA KUPAMBU.

BAADHI ya wananchi wa kijiji cha Bulekela kata ya Masanga  wilayani Kishapu  wameukataa mradi wa maji uliotengewa jumla ya shilingi millioni 28.5 kwa madai  ya  kutoshirikishwa na wataalamu  huku  wakitaka mabomba yasambazwe karibu na nyumba zao  na sio visima virefu au vifupi vya kupampu na mkono ambapo madiwani wameazimia kuondoa mradi huo katika kijiji hicho.


Wananchi hao wameshauri na mkuu wa wilaya Wilson Nkhambaku ,mkuu wa mkoa  Ally Rufunga waupokee  mradi huo kwa uwepo wake  kwenye kijiji chao lakini bado wameonyesha kutokubaliana nao  na kudharau ushauri huo kinachotakiwa ni kumtaka mkurugenzi kuhamisha mradi na kupeleka maeneo mengine  ambako wanashida ya maji.

Hayo yalibainishwa kwenye kikao cha baraza la madiwani na baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo huku diwani wa kata ya Masanga Shiboka  Pombe akitoa kilio chake  kwa wananchi wa kijiji hicho, ambapo  mradi wa maji wananchi wamekuwa wakiukataa kutokana na sababu hizo pia kwa kupinga  wataalamu walivyobaini .

Diwani  huyo alisema kuwa  zilitengwa jumla ya shilingi Mill 28.5   kwaajili ya kuchimba  visima virefu lakini maji yalipokosekana kwa mujibu wa wataalamu akiwemo  mhandisi wa maji Lucas Saidi  waliamua  viwekwe  visima vifupi  viwili kwa fedha hizo kwa  kijiji hicho kimoja  vitakavyotumia pampu ya mikono.

Pia diwani wa  kata ya  Mwamashele Julius Kwihuja  alisema kuwa  maazimio yalikuwa  mradi huo uhamishwe  kwani maeneo mengi wananchi wanateseka kwa kukosa huduma ya maji  wao  wamepata kiburi  kwanini wambembelezwe  ikiwa hata kwenye kamati  suala hili limezungumzwa kuwa mradi huo uhamishwe wanajivunia kuwa karibu na mto.

“Wananchi wa kijiji cha Bulekela  wamekataa mradi wa maji,ikiwa mkuu wa wilaya,mkoa  wameenda kuwashauri lakini bado wanakataa kwanini mradi huo usihamishwe  wakati maeneo mengi hayana huduma ya maji  wamekuwa na kiburi sababu ya kuwa karibu na mto hivyo kwanini pia  tuwabembeleze hata kwenye  kamati tumekwishalizungumza  kuwa mradi huo uhamishwe……”alisema diwani Kwihuja. 

Hata hivyo mwenyekiti wa  halmashauri hiyo  Justine Sheka alisema kuwa utafiti uliopatikana hapo kuwa eneo hilo  maji ni kidogo ila eneo walilochimba kisima maji yapo kwa wingi  ila wao bado hawataki  hata mradi ukihamishwa tayari kunahasara  manunuzi ya pambu ni shilingi million saba,gharama ya uchimbaji shilingi million 20 tayari zimekwisha tumika.

Pia mhandis wa maji Saidi  alisema kuwa walipopima eneo hilo  walibaini  maji ni kidogo kwa kutotosheleza mtandao wa maji ya pomba kwa kitaalamu   hivyo wakashauri kuwa kuwekwe visima vifupi vya pambu ya mikono lakini wananchi walipoelezwa walikataa na kutaka mabomba yatakayo sambaaa mpaka majumbani mwao.

Naye mkurugenzi wa halmashauri hiyo  Jane Mwitagurwa alisema kuwa  malalamiko yaliyopo dhidi ya wananchi kuwa wakati wataalamu wanapima hawakushirikishwa na wataalamu,hivyo mpango wa upimaji uanze upya  kwa kuwashirikisha ikiwa utaratibu wa kusambaza mabomba  ufanyike,wanachokataa kingine ni ile shida ya kupampu kwa mkono.

“Kuhamisha mradi huo utaleta tena gharama kubwa  hakuna fedha  kinachotakiwa  ni kuondoa  mgogoro uliopo,mpango wa upimaji uanze upya  kwa kuwashirikisha  wananchi na usambazaji wa  maji kwenye mambo ufanyike shida yao hawataki visima hivyo ambavyo vya kupampu kwa mkono ndicho kilichobainika kwenye kijiji hicho”alisema mkurugenzi  Mwitagurwa.

KARENY. Powered by Blogger.