Habari za hivi Punde

DREVA WA DALADALA YA BAISKELI MANISPAA YA SHINYANGA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KOSA LA KUBAKA MTOTO WA MIAKA MINANE,KUMLAWITI KISHA KUMTOBOA MACHO,MAHAKAMA IMETOA ADHABU YAKE.

MAHAKAMA  YA HAKIMU MKAZI  MFAWIDHI MKOANI  SHINYANGA 
DREVA wa daladala ya baiskeli  aliyekuwa akikabiliwa na tuhuma   dhidi  ya  ubakaji na kulawiti watoto katika Manispaa ya Shinyanga amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kesi tatu tofauti.
Mtuhumiwa huyo Jacob Mayani au maarufu kwa jina la Boy mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa manspaa ya Shinyanga  amehukumiwa vifungo vitatu vya maisha kwenye MAHAKAMA ya  Hakimu mkazi Mfawidhi Shinyanga.
Jacob Mayani ambae alituhumiwa kuhusika na  matukio tofauti ya ubakaji na kulawiti watoto chini ya maiaka 10 sanjari na kuwatoboa macho amejikuta akiishia gerezani.
Kabla ya kutolewa hukumu ya tatu ya kifungo cha maisha wiki hii na mh Hakimu mkazi mfawidhi John Chaba tayari mtuhumiwa huyo alikua ameshahukumiwa vifungo vingine  viwili vya maisha kwa kesi za ubakaji na ulawiti 
.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Chaba amesema ameridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka dhidi ya mtuhumiwa huyo na adhabu hiyo itakua fundisho kwa Mayani na wengine.
Awali ilidaiwa na upande wa Mashitaka ukiongozwa na wakili wa serikali Salome Mbuguni kwamba  Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo February 12 mwaka jana majira ya saa kumi jioni katika kijiji cha Mwamashele Kizumbi Manispaa ya Shinyanga kwa kumbaka mtoto huyo wa darasa nne.
 Upande huo wa mashitaka ulidai kwamba mtoto huyo alikua ametumwa mandazi na mama yake mdogo ndipo alipokutana na mtuhumiwa njiani na kumrubuni aende nae akampatie mzigo wa bibi yake ndipo alipofanya kitendo hicho.
Mbali na vifungo hivyo vitatu vya maisha gerezani  Mayani anakabiliwa na kesi ingine ya kubaka pamoja na tuhuma ya kutoboa macho watoto kesi ambayo itasikilizwa na mahakama Kuu baada ya upelelezi kukamilika

kwa mwaka jana kuliibuka matukio ya ubakaji na kulawitiwa  watoto pamoja na  kutobolewa  macho kwa kasi kubwa  manspaa ya Shinyanga Jambo ambalo liliwaweka wazazi na watoto  kuishi kwa hofu.
KARENY. Powered by Blogger.