Habari za hivi Punde

JOHN SHIBUDA;CHADEMA WALINIAHIDI UONGOZI NA KUTEMBELEA HELKOPITA MAMBO YAMEENDA KINYUME.

Siku moja baada ya Mbunge wa Maswa Magharibi John Shibuda kutanga kuachia ngazi ndani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHEDEMA) mbunge huyo ameibuka tena na kusema kuwa alihadiwa kupewa ndege 2 (helkopita) na uongozi wa chama hicho lakini mpaka sasa hajapewa.


Shibuda alisema kuwa uongozi wa chama hicho ukiongozwa na Katibu Mkuu Willbrod Slaa ulimuhadi kumpa ndege hizo wakati wa kipindi cha kampeini mwaka 2010 kwa ajili ya kumpigia kampeini katibu huyo wakati akiwania nafasi ya uraisi.

Alisema kuwa katika kipindi hicho mbali na kuhaidiwa ndege hizo, alikuwa chanzo cha mgombea huyo kuwa na kura nyingi kwa mara ya kwanza chadema kuogoza Wilaya ya Maswa na kumzidi mgombea mwenzake aliyekuwa chama cha mapinduzi CCM Jakaya Kikwete.

Mbunge huyo wakati akiongea na wananchi katika kata ya Malampaka Wilayani Maswa Mkoani Simiyu alisema kuwa alijitolea kwa kutumia pesa zake katika uchaguzi huo na kuadiwa kurudishiwa, lakini mpaka sasa hajawahi kurudishiwa pesa hizo.

Aidha aliongeza kuwa ndege hizo alizohaidiwa kwa ajili ya kufanyia kampeini hajawahi kuletewa na hata wakati wa kampeini hakupewa, huku akibainisha kuwa alipoulizia aliambiwa kuwa atapewa.

“mimi ndiye chanzo kikubwa cha Jakaya Kikwete kushindwa kwa kiwango kikubwa katika jimbo langu na wilaya ya maswa kwa ujumla…nilitumia gharama zangu kumfanyia kampeini Dk Slaa..nikaambiwa nitarudishiwa mpaka sasa sijaziona…hizo ndege mpaka leo zijaziona..lakini ninatukanmwa” Alisema Shibuda.

Wakati huo huo mbunge huo alibainisha kuwa msimamo wake ni serikali mbili, huku akibainisha kuwa hawezi kuunga mkono msimamo wa UKAWA wa serikali 3 ili kuwaongezea mgizo wananchi wake ambao ni wakulima na wafugaji.

Alisema kuwa wananchi wake hawataki kuongezewa mzigo wa serikali bali wanataka kutatuliwa kero walizonazo hasa katika kilimo cha pamba pamoja na migogoro ya wakulima na wafugaji.

“siko tiyari kuunga mkono serikali 3 kwa sababu wakulima wa pamba wanamatatizo makubwa juu ya bei, pamoja na pembe jeo, lakini wilaya yangu ya maswa kuna migogoro mikubwa ya wakulima na wafugaji..inatakiwa kutatuliwa kwa serikali hii tuliyonayo” Alisema.

Aidha mbunge huyo alienda mbele Zaidi kwa kumfananisha Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu na mauaji ya kimbali ya nchini Rwanda (INTERAHAMWE) kwa kuwa amekuwa mchochozi wa vita ndani na nje ya chama.

“Tundu Lissu ni INTREHAMWE…amekuwa mtu wa choko choko na tabia ya kuwatukana wenzake..huyu hana tofauti na mauaji hayo..maana waliosababisha walikuwa watu wenye choko choko na uchochezi mkubwa kama alivyo yeye” Alisema.

0 Response to "JOHN SHIBUDA;CHADEMA WALINIAHIDI UONGOZI NA KUTEMBELEA HELKOPITA MAMBO YAMEENDA KINYUME."

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.