Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na
Ushirika Godfrey Zambi juzi nusuru apate kipigo kutoka kwa wakulima wa pamba
katika kijiji cha Marekano Kata ya Kadoto Wilayani Maswa Mkoani Simiyu wakati
alipowatembelea wakulima hao, kwa kile kilichodaiwa kupewa majibu yasiyo
ridhisha juu ya Mbegu za Quton.
Wakati akiotoa majibu kwa wakulima
hao ambao waliokusanyika gafla katika kituo cha kukusanyia pamba
alichokitembelea kukagua mizani inayotumika kupima zao hilo, wakulima hao
walianza kumzomea Naibu waziri huyo wakati akiongelea Mbegu hizo pamoja na bei
ya pamba.
Wakulima hao walitaka kujua hatima
yao juu ya kupewa fidia kwa wale ambao walitumia mbegu hizo, ambazo haizkuota
na kuwasababishia hasara kubwa, ikiwa pamoja na kutaka kujua mipango iliyopo ya
serikali kuwadhibiti wafanyabishara wanaowaibia kupitia mizani ya Digital.
Wakati akitoa majibu hayo Zambi
alianza kuzomewa na kutaka kupigwa na wakulima hao, baada ya kutoridhika na
majibu yaliyokuwa yakitolewa na kumtaka aondoke katika eneo lao kwa kile walichodai
kuwa serikali imeshindwa kuendeleza zao la pamba.
Wakiongea kwa hasira wakulima hao
walimtaka naibu waziri kuifuta bodi ya pamba (TCB) kwa kile walichokidai kuwa
wamekuwa wakiteseka na kuangaika bila ya kuhurumiwa katika kupanda, kuvuna hadi
kuuza zao hilo.
Walisema bodi ya pamba imekuwa
chanzo cha zao la pamba kuporomoka pamoja na kusababisha umaskini mkubwa kwa
wakulima wa zao hilo, kwa kuwanyonya katika bei yake ikiwa pamoja na
kuwaletembea mbegu mbovu.
“tunaomba uondoke hapa…hatukutaki hata
kidogo..serikali mmetonyonya sana wakulima wa pamba na tunaomba ukiondoka hapa
ondoika na bodi ya pamba na mbegu hizo za Quton hatuzitaki hata kidogo”
Walisema wakulima hao.
Wakati wakulima hao wakimfukuza
Naibu Waziri Mbunge wa Bariadi Magharibi John Shibuda aliwatuliza wakulima hao
na kuwazuia wasimpigi wazari ambapo aliwaondoa katika eneo ambalo waziri
alikuwepo na kuwapeleka mbali.
|
0 Response to "SHIBUDA AMNUSURU NAIBU WAZIRI WA KILIMO NA CHAKULA KUTAKA KUSHUSHIWA KIPIGO NA WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA."
Post a Comment