Siku chache baada ya Mbunge wa Maswa
Magharibi John Shibuda (CHADEMA) kudaiwa kuusaliti Umoja wa Katiba ya Wananchi
(UKAWA) kwa kurudi katika bunge la katiba linaloendelea na vikao vyake mjini
Dodoma, na kuwepo taarifa za kufukuzwa ndani ya Chama chake (CHADEMA) Mbunge
huyo imeibuka na kusema kuwa amechoswa na Chama hicho.
Chibuda amesema kuwa amechoka
kutukanwa, kuitwa msaliti, mnafiki huku akibainisha kuwa kamwe hawezi kuvumilia
vitendo hivyo na kubainisha kuwa matusi ambayo yametolewa juu yake sasa
yametosha.
Mbunge huyo aliyasema hayo jana
wakati akiongea na waandishi wa habari pamoja na Baraza la wazee Wilayani Maswa
Mkoani Simiyu, na kutangaza rasmi kuachana na chama hicho.
Alisema tangu amejiunga na chadema
amekuwa mtu wa kutukanwa na kuitwa masaliti kila mara, ikiwa pamoja na kunyimwa
ushirikiano kutoka katika uongozi wa juu wa chama hicho katika kukiletea
maendelea na wananchi kwa ujumla.
Alibainisha kuwa chadema kimeshindwa
kumpa heshima aliyona nayo, hivyo kubainisha kuwa hawezi kuendeshwa kama mtoto
na wala kupelekwa kama viongozi wa chama hicho wanavyotaka.
“tangu nimejiunga chama hiki..kila
siku ni matusi kwangu..hata watoto wadogo ndani ya chama hiki nao wamediriki
kunitukana..sasa nimechoka na siwezi kuvumilia hali hii..nimekuwa mvumilivu kwa
muda mrefu..natanga kuwa sitagombea ubunge nikiwa Chadema na cha hiki siyo baba
wala mama yangu” Alisema Shibuda.
Kuhusu kurudi Bungeni.
Akiongelea juu ya taarifa za kurudi
bungeni mwanasiasa huyo alisema kuwa taarifa hizo siyo za kweli na hajawahi
kuingia ndani ya bunge hilo, bali alipita wakati akitokea Dar es Salaam kwa
ajili ya kupatiwa matibabu.
Alibainisha kuwa wakati akitokea
mkoani Dar es Salaam afya yake ilikuwa mbaya, ikiwemo kuvimba miguu, hali
iliyomlazimu kupia kupita kwa madaktari walioko ndani ya viwanja vya bunge ili
kupewa dawa na kuangaliwa afya yake.
“wakati nipo njiani nakuja Maswa
kwenye Msiba afya yangu ilikuwa mbaya..nikaamua kumpigia simu daktari pale
bungeni juu ya afya yangu..akaniambia nipite akanicheki..nilipofika bungeni
nikapewa maelekezo ili niweze kupata dawa na kuangaliwa afya yangu ni lazima
nijiandikishe” alisema na kuongeza kuwa..
“nami sikukataa kujiandakisha
nilipomaliza utaratibu wa kujiandikisha nilipewa dawa na kuangaliwa afya yangu..na
watu waliponiona hapo bungeni wakasema nimewasaliti UKAWA jambo ambalo siyo
kweli”
Alisema alipomaliza kupata dawa
aliendelea na safari yake kuja katika jimbo lake kwa ajili ya msiba, ambapo
alieleza kushangaa kusikia kuwa karudi bungeni wakati yuko msibani.
Kuhusu UKAWA.
Akiongelea juu ya Umoja wa Katiba ya
Wananchi (UKAWA) waliogoma kurudi bungeni, Shibuda alisema kuwa umoja huo hauna
maslai kwa watanzania ambao alisema asilimia kubwa ni wakulima na wafugaji.
Alibainisha kuwa tangu watoke ndani ya
bunge hilo na yeye akiwa mmoja ya waliotoka, hajawahi kujulishwa jambo lolote
juu ya mwenendo wa mazungumzo baina ya umoja huo na CCM.
Alisema kitendo cha kutojurishwa
jambo lolote kimekuwa kikimpa shida ya kuamua kuendelea na bunge au kususia, kutokana
na kutopewa taarifa za mchakato wa maridhiano, huku akibainisha kuwa wajumbe
wengine wamekuwa wakipata taarifa hizo na yeye kubaguliwa.
“mimi siyo mkokoteni..na siwezi
nikaota juu ya maamuzi ya UKAWA ambayo wamekuwa wakiyajadili katika vikao vya
maridhiano..wajumbe wengine wamekuwa wakipewa taarifa kila siku na
kinachoendelea mpaka sasa…lakini mimi nabaguliwa kwa nini?” Alisema
Aidha aliuponda umoja huo kwa kusema
kuwa hauna maslai kwa wakulima wa pamba, pamoja na wafugaji, ambao alisema
ndiyo wapiga kura wake na ambao walimtuma bungeni kujadili kero zao.
Atangaza kurudi bungeni.
Katika hali isiyo ya kawaida Mbunge
huyo alitangaza rasmi kuendelea na vikao vya bunge maalumu la katiba, kwa madai
kuwa anaenda kuzungumzia kero za wakulima wa pamba pamoja na wafugaji ili
ziwekwe katika katiba mpya.
“mimi nipelekwi pelekwi…na wala siko
tayari kupelekwa na chama chochote hapa nchini wala viongozi..nasema nitaenda
bungeni wiki hii..kuendelea na vikao niwatetee wakulima wangu wa pamba pamoja
na wafugaji ambao ni maskini sana” Alisema.
Juu ya viongozi wa Chadema.
Akiongelea juu ya uongozi ndani ya
chama hicho alisema kuwa viongozi wamekuwa wakitumia ubabe, vitisho, pamoja na
ubaguzi katika kukiendesha chama, huku akieleza kuwa viongozi hao wamekuwa hawana
hekima na busara.
Alibanisha viongozi hao wamekuwa
wakitumia ubabe na kuwaendesha wanachama wao pamoja na wabunge wao kama watumwa
na kuwataka kufanya watakavyo kwa maslai ya kwao binafsi.
“chadema viongozi wote ni wababe,
hawana hekima na busara wanataka kuendesha chama watakavyo, kama cha
kwao...mimi hiyo nimekataa. nataka niwaambie viongozi hao waliposikia nimetoka
CCM wao ndiyo walinifuata nijiunge na chama chao” Alisema
Atangaza vita dhidi ya Tundu Lissu.
Akiongea kwa asira kali, mbunge huyo
alibainisha kukerwa na mwanasheria wa chama hicho na mbunge wa Singida
Mashariki Tundu Lissu, kwa kuendelea kumwandama bila ya sababu maalumu na
kumtaka kuacha mara moja vitendo hivyo.
Alisema amemvumilia kwa kiwango
kikubwa mbunge huyo, ambapo alitangaza kuanzisha vita dhidi yake juu ya
kinachoendelea katika kumuongelea uongo mbao hauna faida yeyote.
“Lissu amenishtumu mengi
nimemsikiliza sana..na nimemvumilia vya kutosha..sasa ndani ya siku chache
nikirudi Dar es Salaam tutaonana..maana mimi siwezi kutukanwa na mtoto mdogo
kama Lissu” Alisema.
Shibuda mbali na kutangaza kukiama
chama hicho hakuwa tiyari kuzumgumzia chama atakachoamia, ambapo alibainisha
kuwa chama atakachoamia bado ni siri yake, huku akibainisha kuwa kitakuwa chama
kipya hapa nchini.
Wazee wamuunga mkono.
Nao wazee waliohudhulia Mkutano huo
walimuunga mkono mbunge huyo kwa uhamuzi wake wa kikiama chama hicho, huku
wakimtaka kurejea bungeni kwa ajili ya kutetema wananchi wa maswa ambao ni
wakulima na wafugaji.
“sisi kama wazee tunakuunga mkono
mbunge wetu..na tunawataka wabunge wengine kurejea bungeni kujadili matatizo ya
watanzania..watanzania matatizo yao siyo muundo wa serikali..tunataka wakulima
na wafugaji wadhaminiwe” Alisema Mohamed Mangasiri Mwenyekiti Baraza la wazee
Maswa.
|
0 Response to "MBUNGE JOHN SHIBUDA ATOA YA MOYONI MWAKE,ATANGAZA VITA DHIDI YA TUNDU LISSU."
Post a Comment