Habari za hivi Punde

SHULE YA MSINGI KANO MADAWATI 65 SHULE NZIMA WANAFUNZI ZAIDI YA 500

Hili ni darasa  la tatu katika shule ya msingi Kano iliyopo katika kijiji cha Amani kata ya Salawe  halmashauri ya wilaya ya Shinyanga   kama inavyoonekana  madawati yake wanafunzi walikwisha haribu na kuendelea hivi sasa kukaa chini,hata fedha za kutengeneza hayo zimekosekana kwa wazazi ambao wanadai kuwa  na hali ngumu kifedha hivyo wanaiomba serikali kuangali suala hili  huku wakidai  mzigo huo umekwisha washinda.

Hili ni darasa la pili katika shule hiyo  ambapo wanafunzi hukaa zaidi ya 60 darasa moja ambapo hupeana zamu ya kukaa kwenye madawati kutokana na changamoto pindi wanapoandika  miandiko yao huwa mibaya  na kuwafanya walimu kupata ugumu katika usahihishaji wa madaftari yao.

Hii ndio shule ya msingi Kano  katika kijiji cha Amani  huu ni muonekano wake kwa nje.

Huyu ni mwenyekiti wa kijiji cha Amani Dotto Polepole  akielezea changamoto mbalimbali katika shule hiyo kwa kukosa madawati na kuwafanya wanafunzi  kuendelea kukaa chini,ambapo anaeleza kuwa katika kikao cha serikali ya kijiji wamepitisha azimio la kila  kaya kuchangia madawati  ili wanafunzi wapate japo elimu bora kwa unafuu huo.

Hili ndio jengo la utawala katika shule ya msingi kano ambapo  mlango wa kwanza ni ofisi ya walimu ambapo kwa hivi sasa kuna walimu kumi na moja ila nyumba za walimu zipo mbili na wengine huishi mbali na shule ilipo,mlango unaofuata ni ofisi ya mwalimu mkuu wa shule hiyo  Shabani Masuma

Hili ni darasa la saba  ambalo nlo linawanafunzi  zaidi ya 60  ambapo hupeana zamu kukaa kwenye madawati

Huyu ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi  Kano  Shabani  Masuma akiangalia uchimbaji wa kisima cha maji katika shule hiyo huku akisema kuwa shule hii inachangamoto  kubwa tatu ambazo ni maji,madawati pamoja na  chakula cha mchana kwa wanafunzi ambapo kuna  wanafunzi zaidi ya 500  na madawati yaliyopo ni 65 jambo ambalo linawafanya wanafunzi kukaa chini huku miandiko yao ikiwa mibaya,suala la maji wanafunzi wanateseka sana kwa upande wa kupata maji ya kunywa hukaa na kiu mpaka watakapo rudi majumbani kwako pia chakula cha mchana kimekuwa ni tatizo  hivi sasa kilicholimwa shuleni hapo kimeisha na wazazi katika uchangiaji wanadai mwaka huu hawakuvuna na hata pesa hawana hiyo nayo ni changamoto ikiwemo utoro kwa wanafunzi zaidi ya wanafunzi 40 hawahudhurii masomo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo wazazi wao ni wafugaji hupelekwa kulisha mifugo na kuhamahama.

Mwenyekiti wa kijiji cha Amani Dotto akiwa pamoja na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kano Shabani Masuma.

Wanafunzi hawa sio kwamba wamepata adhabu kutoka kwa walimu    wamekaa chini huku somo likiendele kwa changamoto ya uhaba wa madawati shuleni hapo.

Hiki ni kikao cha serikali ya kijiji cha Amani kata ya Salawe halmashauri ya wilaya ya Shinyanga  ambapo  hoja mbalimbali zilikuwa zikielezwa ikiwemo uchangiaji wa madawati kwa kila kaya ili kuweza kupata angalau madawati 30 kwaajili ya wanafunzi wa shule ya msingi  Kano,ambapo mjumbe kwenye kamati hiyo  Zoya Mstapha alisimama na kuchangia hoja kwenye kikao hicho.

0 Response to "SHULE YA MSINGI KANO MADAWATI 65 SHULE NZIMA WANAFUNZI ZAIDI YA 500"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.