Habari za hivi Punde

KUNDI LA PANYA LAMSHAMBULIA MTOTO WA MWEZI MMOJA VIUNGO VYAKE VYA MWILI.

Taarifa kutoka mjini Johannesburg Afrika Kusini zinasema - kuwa panya walimng'ata mtoto wa mwezi mmoja vidole na pua .
Mtoto huyo anasubiri kufanyia upasuaji wa kuumba maumbile yake ya usoni baada ya tukio hilo huko Alexandra, Johannesburg .
Panya walimvamia Erena Yekanyi nyumbani kwao katika kitongoji duni cha Alexandra.
Wazazi wake wanasema kuwa haWana fulusi za kumpeleka hospitalini kwa matibabu anayohitaji kwa haraka baada ya kunga'twa jumatatu.
“nilikuwa nafua hapo nje naye Erena alikuwa ndani amelala.Mara nikamsikia akilia ndipo nikakimbia ndani kuangalia kulikoni ,,,nilimpata anafuja damu ''alisema mamake Thandaza.
Sasa mtoto huyo anasubiri kufanyiwa upasuaji ambao utaumba upya pua lake na pia vidole vitatu vilivyong'atwa .
Mamake anasema madaktari katika hospitali ya Charlotte Maxeke Academic Hospital wanasubiri achangishe pesa za kutosha operesheni hiyo.
Kulingana na ripoti hiyo tukio hilo sio la kwanza katika makazi hayo duni.
Inadaiwa kuwa watoto wengi na wazee wameripotiwa kung'atwa na panya hao wanaoonekana sio wa kawaida kutokana na kimo chao.
Msemaji wa mji wa Johannesburg Nkosinathi Nkabinde panya ni wengi katika mitaa hiyo kutokana na hali duni ya usafi.
Amesema kuwa kunamipango ya kuangamiza wanyama hao.
 CHANZO:BBC
KARENY. Powered by Blogger.