Habari za hivi Punde

KIKONGWE AUWAWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA, ACHARAZWA MAPANGA.


Kikongwe mwenye umri wa miaka 62 Raheli Jilungu mkazi wa kijiji cha Mishepu katika halmashauri ya wilaya ya  Shinyanga aliuawa kwa kukatwa shingo na mtuhumiwa aliyetambulika kwa jina la Maganga Fuja akiwa na wenzake
watatu .Chanzo cha mauaji hayo ni imani potofu za  kishirikina. 

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga  Justus Kamugisha atoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga kupambana na vitendo vya mauaji ya vikongwe.Kamugisha alisema kazi kubwa hivi sasa kwa upande wake kuhakikisha mauaji yanakoma mkoani Shinyanga.alisema ufanisi wa mapambano hayo  yanategemea  ushirikiano kutoka kwa wakazi wa mkoa wake kwa kutoa taarifa za wausika wa mauaji hayo.alisema mauaji hayo yamekuwa na mtandao mkubwa wakiwemo ndugu wa marehemu wanaofanyiwa vitendo hivyo. 
Pia  kuanzia Januari mpaka desemba  mwaka 2013  mkoa ulikuwa na mauaji ya vikongwe 27 huku watuhumiwa 16 wakifikishwa mahakamani na kuanzia mwezi Januari hadi  Julai mwaka huu vikongwe 11 wameuwawa huku watuhumiwa 16 pia wakifikishwa mahakamani.

KARENY. Powered by Blogger.