Habari za hivi Punde

RACHAL MASHISHANGA AUKWAA UENYEKITI BAWACHA MKOA WA SHINYANGA CHADEMA

HUYU HAPA NI RACHAL MASHISHANGA  MBUNGE VITI MAALUMU CHADEMA MKOANI SHINYANGA AMEUKWAA UENYEKITI WA BAWACHA  CHADEMA MKOA.CHAMA  Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA),mkoani Shinyanga hatimaye kimepata viongozi wapya wa mkoa ,ikiwa imepita miaka mitatu bila ya kuwa na mwenyekiti wa mkoa wa Chama hicho ikiwa  wamemchagua  Peter Frank kuwa mwenyekiti kushika nafasi ya aliyekuwa  mwenyekiti  phlipo Shelembi aliyefariki  dunia mwaka 2011.

Akisimamia uchaguzi huo Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki  (CHADEMA),Sylivester Kasulumbai, uliofanyika Mjini Shinyanga, alisema lengo la uchaguzi ni kuendelea kukiimarisha chama  na kujipanga katika chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2015,kwakuhakikisha  wanaiongoza nchi.

Kasulumbai aliwataja viongozi hao wapya waliochaguliwa, huku  katibu wa mkoa  Zacharia Thomas, Mwenyekiti wa Vijana (Bavicha), Chripin Simon, Katibu wake Ezekiel Joseph.

Mwenyekiti wa akina mama (Bawacha), Rachel Mashishanga,  ambaye pia ni Mbunge wa viti maalum (CHADEMA),Jimbo la Shinyanga Mjini huku katibu wake akiwa Wilfrida  Daudi ,na Mwenyekiti wa wazee mkoa Mhidini Ibrahimu.

Kufuatia uchaguzi huo ambao ulifanyika kwa amani ,Kasulumbai aliwataka viongozi hao wapya (CHADEMA),mkoa kufanya kazi kwa ushirikiano bila ya kuwa na makundi ikiwemo  kuzingatia sera na katiba ya Chama.

“Mmechaguliwa kuwa viongozi wapya wa mkoa ,hivyo nawataka mfanye kazi kwa ushrikiano pamoja na kuzingatia kanuni ya katiba ya Chama, tukiwa na mshikamano wote, lazima chama chetu kitasonga mbele na kujenga imani kwa watanzania ambao watatupa ridhaa ya kuinga Ikulu 2015.”alisema Kasulumbai

 

0 Response to "RACHAL MASHISHANGA AUKWAA UENYEKITI BAWACHA MKOA WA SHINYANGA CHADEMA "

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.