BAADHI ya makampuni ya ununuzi wa zao la pamba mkoani
Shinyanga yameonesha kujitoa kuendelea na ununuzi huo kwa kudai kuwa soko
la dunia limeshuka hawatapata faida ambapo chama kikuu cha ushirika
mkoani humo( Shirecu) kimeendelea na ununuzi huo na kufikia kilo millioni
4.8 ikiwa lengo lake kwa mwaka huu ni kufikia kilo zaidi ya millioni 8.
Mojawapo ya kampuni lililojitoa na ununuzi huo ni kampuni ya Ahamu kwa kuona
itapata hasara ambapo asilimia 75 ya wakulima wamejitokeza kuuza pamba
yao huku asilimia 25 wakisubiri huenda soko litakuwa zuri ikiwa bei iliyopo
hivi sasa ni shilingi 750 kwa kilo moja.
Wakiongea na mwandishi wa habari kwa nyakati tofauti mjini Shinyanga
meneja wa shirecu Joseph Mihangwa alisema kuwa kweli wanunuzi wengi
wamejitoa ila kupitia chama chake wanaendelea kununua na
kufikia kilo millioni 4.8 na malengo ni kilo millioni 8,huku
mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje alisema
wakulima wadogowadogo wamejitokeza kuuza lengo kupata fedha na kukithi
mahitaji ndani ya familia.
‘Shirecu kwa malengo hayo inatarajia kuyafikia ikiwa makampuni mengine
yamejitoa sifahamu sababu ni kitu gani kujitoa kwao,lakini soko la
dunia limekuwa baya kwa kuangalia bei iliyopo hata hii ya
shilingi 750 tunayonunua kutoka kwa mkulima ni kubwa hivyo
tunanunua kwa matumaini huenda soko la dunia bei yake ikawa
nzuri”alisema.
Mihangwa alisema kuwa changamoto ya mizani kwa upande wao hakuna tatizo
kwani imekuwa ikisimamiwa na vyama vya msingi vya ushirika kwa usahihi
ikiwa kuna vyama 480 vilivyochini ya shirecu ambapo kati ya hivyo 210
vilivyojiimarisha kwenye biashara huku vilivyobaki vimeteteleka
kutokana uchumi wake kutokuwa mzuri.
Naye Ngassa Mboje alisema kuwa baadhi ya wakulima
wakubwa wa zao la pamba hawajajitokeza kuuza wakisubiri soko kuwa zuri
huku msimu ukienda mwishoni, lakini wakulima wadogo waliowengi
wamejitokeza kuuza kwa bei ya shilingi 750 lengo waweze kupata fedha za
kujikimu ndani ya familia zao.
Hata hivyo Diwani wa kata ya Mondo wilayani Kishapu mkoani
Shinyanga John Ndama alisema kuwa wakulima wamekosa
ujanja imebidi wauze kwa bei hiyo ikiwa kampuni inayojulikana
Villani ilianza kununua pamba kwenye baadhi ya maeneo kwa shilingi 800
kwa kilo moja ambapo kampuni ya jambo ilijitoa na baadaye kurudi na
kampuni ya Ahamu imekwisha jitoa jumla kwenye ununuzi huo.
Nao wakulima wa zao la pamba mkoani Shinyanga
akiwemo Maduhu Shija na Bernadetha Joshua walisema kuwa
wakulima wamekubali kununua kwa bei ya shilingi 750 kwa kilo kutokana na
changamoto kubwa ndani ya familia ,hata kujitoa kwa baadhi ya
makampuni kununua zao hilo wako sahihi kwani wameona wanapata
hasara pia.
|
0 Response to "MAKAMPUNI YA UNUNUZI WA ZAO LA PAMBA YAONJA JOTO YA JIWE SOKO LA DUNIA."
Post a Comment