WAKIBEBA ZAO LA DENGU NA KUPELEKA NYUMBANI KWA KUCHAMBUA.
WAKULIMA wa zao la dengu katika kijiji cha Amani kata ya Salawe halmashauri ya wilaya ya Shinyanga bado wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa soko la uhakika kwenye zao hilo ikiwemo miundombinu ya barabara kuwa mibovu hali ambayo
inawafanya kushindwa kusafirisha mazao yao.
Wakiongea na mwandishi
wa habari aliyetembelea wakulima wa kijiji hicho walisema kuwa zao hilo limekuwa mkombozi katika kunyanyua
pato la familia lakini kubadilika kwa bei ikiwa wengine wanauza shilingi
45,000 mpaka 55,000 kwa gunia moja na kukosa soko la uhakika imekuwa ni tatizo, ikiwemo wadudu wahalibifu pamoja na panya.
Wakulima kutoka kijiji cha Amani Josephati Mahona na Mariamu Kihembe walisema kuwa changamoto imekuwepo, wakati wa kukomaa kwa zao hilo likiwa shambani kwa kuliwa na
wadudu ambapo hutumia gharama ya kiasi cha shiling 6000 kununulia dawa za kuua wadudu.
“Kwa kweli zao hili ni
mkombozi kwenye familia hakuna zao lingine tunalolitegemea linalokomaa kwa muda
mfupi na kuuza,lakini kumekuwepo na changamoto ya soko kukosa uhakika, wakulima tumekuwa
tukijitafutia soko kama kuku wa
kienyeji serikali imetusahau,pia hata hawa walanguzi wamekuwa wakitudhulumu kwa
kiasi kikubwa ikiwa nasi tumetumia gharama kubwa katika maandalizi”alisema
Mahona.
Naye Twiga Mashimba mkulima wa zao hilo alisema kuwa zao la dengu linaanza kulimwa mwezi march na mavuno
yake ni kipindi cha kuanzia mwezi wa saba hivyo changamoto za usafirishaji na soko kubadilikabadilika
kumekuwa kukimnyima fursa mkulima kufahamu bei halisi kwani walanguzi wao huenda kuuza kwa gharama
ya shilingi 70,000 kwa gunia moja.
Mwenyekiti wa kijiji cha
Amani
Dotto Polepole alisema kuwa licha ya wakulima
kulilima zao hilo na kutegemea kuongeza kipato ndani ya familia kumekuwa na
changamoto ya kuwepo kwa miundombinu
mibovu kwenye usafirishaji wa mazao ambapo wakulima wengi wamekuwa wakipeleka
jijini Mwanza na kuona ndio karibu na
unafuu kwao kuliko shinyanga mjini.
Ofisa kilimo wa
halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Oscar Jeremiah alisema kuwa zao hilo linaathiriwa na
unyevunyevu liwapo ardhini na hufanya kuoza ikiwemo wadudu wahalibifu kama
funza na panya hiyo imekuwa ni
changamoto.
Ofisa kilimo huyo
alisema kuwa kilimo cha zao la
dengu
kinaanza mwezi March
kipindi mvua zimeanza kupungua kwani linahitaji mvua za
wastani, kwa mwaka huu matarajio
yalikuwa ni kulima hekta 8,644 na mavuno tani 5,108 lakini imefikia katika
uhalisia eneo lililolimwa kwa
mwaka huu ni hekta 3,881 na mavuno halisi ni tani 2,293.
|
0 Response to "CHANGAMOTO YA KUKOSA SOKO LA UHAKIKA KWA WAKULIMA CHANZO CHA UMASIKINI."
Post a Comment