BAADHI ya wananchi manispaa ya Shinyanga wametakiwa kuwapatia elimu
zaidi vijana na kuondoakana na uhalifu ambao chanzo chake ni utumiaji
wa madawa ya kulevya, biashara ya vyuma chakavu ikiwemo wizi wa nyaya za simu
hali ambayo imefanya shirika la mawasiliano ya umma nchini TTCL kwa
wilaya shinyanga kupata hasara ya zaidi ya shilingi million 133.
Suala
la unyang’anyi na wizi kwa vijana kwenye maeneo ya makazi limekithiri
hasa kwenye upande wa wizi za nyaya za simu ambao umekosa ulinzi, watu
kudiriki kufanya vitendo vya kufua nyaya karibu na makazi hivyo
shirika la TTCL katika eneo la kata ya ndembezi,Ngokolo zilizibiwa
cable urefu wa mita 200 na kupatikana hasara ya zaidi shilingi
millioni sita.
Hayo yalisemwa na naibu meya wa manispaa hiyo
David Nkulila ambaye pia ni diwani wa kata ya Ndembezi pamoja na
ofisa ufundi kutoka shirika hilo Madunda Madunda kwenye mkutano wa
hadhara uliohusisha kata tatu za mjini,Ngokolo na Ndembezi na
kufanyika katika shule ya msingi Bugoyi A iliyopo eneo la mtaa wa
Mbuyuni kata ya Ndembezi.
Nkulila alisema kuwa uhalifu umezidi
kuongezeka sababu ya vijana wengi kujiingiza kwenye utumiaji wa madawa
ya kulevya na biashara ya vyuma chakavu ambao umeipatia hasara TTCL,
aliwata wananchi kuchukua hatua za haraka kuwaonya vijana wao ikiwemo
biashara hiyo ambayo imekuwa ni chanzo kikubwa cha uhalifu kwenye
maeneo mengi.
“Mimi nasema kuwa madawa ya kulevya vijana wengi
wamekuwa wakiyatumia kwa kisingizo cha kukosa ajira, hilo sio kweli
bali wanayatumia ikiwa wazazi na walezi wakishuhudia na mwisho wake
kufanya uhalifu,pia vilabu vya pombe za kienyeji na baa
kutokufungwa bila kuzingatia muda nao unachangia hivyo atakaye kiuka
utaratibu huu achukuliwe hatua za kisheria”alisema Nkulila.
Naye
Madunda katika mkutano huo alisema kuwa nyanya nyingi zimeibiwa ni
zile za kuunganishiwa wateja ambapo alidai kuwa suala la wizi
lilikithiri hali ambayo inaonekana shirika la TTCL linataka kuhujumiwa
kwa njia hiyo, kwani wizi unatendeka maeneo yaliyo karibu na makazi
bila kutoa ushirikiano wa wananchi kwenye eneo husika isitoshe jeshi la
polisi nao wakiwepo. |
0 Response to "WIZI WA NYAYA ZA SIMU WASABABISHA HASARA YA ZAIDI YA SHILINGI MILLIONI 133 MANISPAA YA SHINYANGA."
Post a Comment