Habari za hivi Punde

MBWA AMTAFUNA MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU NA KUPOTEZA MAISHA

Moja ya mbwa anayedaiwa kumla mtoto Ibrahim Faraja Chipungahelo (9) akiwa ameuawa pia.

MWANAFUNZI wa Shule ya Msingi Ludewa mkoani Njombe, Ibrahim Faraja Chipungahelo (9) ameuawa kikatili na mbwa wanaosadikiwa kuwa na kichaa kisha kuliwa nyama. 


Tukio hilo lililoacha simanzi kubwa kwa wakazi wa Ludewa mjini lilijiri saa 7 mchana wa Agosti 8, mwaka huu katika eneo la Ikilu ambapo marehemu na wenzake walikuwa wakipita nje ya nyumba ya mtu aliyejulikana kwa jina la Bosco Lingalangala (Boli) kwenda kuchuma mapera sehemu.
o.
DAKTARI ALIVYOSEMA
Kwa mujibu wa taarifa ya Dokta Sira Rajabu wa Hospitali ya Wilaya ya Ludewa aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu Ibrahim, ulikuwa na majeraha makubwa mwili mzima huku paja la mguu wa kulia likiwa limeondolewa nyama kabisa.
MGANGA WA MIFUGO
Akizungumza na paparazi wakati wa msiba wa mtoto huyo, Mganga wa Mifugo wa Wilaya ya Ludewa, Simon Haule alisema mbwa hao walikuwa hawajapata chanjo kwa zaidi ya miaka miwili. Kwa hiyo tayari walikuwa na ugonjwa wa kichaa ambacho kisingeweza kupona tena zaidi ya kuwaua.

Padri akiiombea roho ya mtoto, Ibrahim Faraja Chipungahelo ikapate kupumzika kwa amani.

WANANCHI WAANDAMANA, WAWAUA MBWA
Kufuatia tukio hilo la kusikitisha, Agosti 10, mwaka huu baadhi ya wananchi wa Kata ya Ludewa waliandamana ili kushinikiza haki itendeke baada ya kuambiwa kuwa mmiliki wa mbwa hao alitishia kumshtaki yeyote ambaye angehusika kuwaua mbwa wake.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano wa dharura ulioitishwa na Diwani Mchilo, wananchi hao walisema mbwa hao walikuwa tishio kwa muda mrefu kwani walishateketeza mifugo mingi wakiwemo mbuzi 22 na ndama 1, lakini cha kushangaza kila walipolipeleka suala hilo kwenye vyombo vya dola, mmiliki alitaka ushahidi.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wananchi hao walisitisha mkutano huo na kuandamana mpaka kwenye nyumba ya mmiliki wa mbwa hao ambapo waliwaua kwa kuwapiga risasi.
MIZOGA MITAANI
Kwa hasira, waliondoka na mizoga na kupita nayo mitaani huku wakiimba nyimbo mbalimbali za kikabila na kawaida.
WACHOMA MOTO MIZOGA
Baada ya kuzunguka na mizoga ya mbwa hao kwa muda mrefu, mwishowe walikwenda kwenye ofisi ya kata ambako waliichoma moto na kuiteketeza kabisa huku wakishangilia.
MKUU WA WILAYA
Kufuatia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Juma Madaha ameviagiza vyombo husika ikiwemo idara ya kilimo na mifugo na jeshi la polisi kuchukuwa hatua za kisheria kwa yeyote anayehusika na tukio hili akiwemo mmiliki wa mbwa hao.
Marehemu Ibrahim Faraja Chipungahelo alizikwa Agosti 9, mwaka huu kwenye Makaburi ya Ludewa, Njombe.

Wananchi wakichoma mwili wa mbwa aliyemuua mtoto Ibrahim.
KAMANDA WA POLISI
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, ACP Fulgensi Ngonyani alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa upelelezi unaendelea sanjari na kuwahoji watu mbalimbali, akiwemo mmiliki wa mbwa hao anayeishi jijini Dar es Salaam.Mungu ailaze pema peponi, roho yake. Amina.

0 Response to "MBWA AMTAFUNA MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU NA KUPOTEZA MAISHA"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.