Habari za hivi Punde

SHIDA YA MAJI WATOTO WASHINDISHWA KWENYE VISIMA,WAZAZI WASAKA MAJI NYAKATI ZA USIKU.

WAKAZI wa kitongoji cha Mwabagikulu katika Kjiji cha  Ikonongo kata ya Salawe halmashauri ya wilaya ya Shinyanga  wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji hali ambayo inawafanya wakazi wa kijiji hicho  kuamka   nyakati za usiku kutafuta maji huku wakiwa na hofu ya kuhatarisha maisha yao,ambapo mkazi mmoja wa kijiji hicho Ndelemo Maguta alisema kuwa inawalazimu kutafuta maji nyakati za usiku  sababu ukienda majira ya mchana hakuna maji  huku watu ni wengi,wengine utakuta wanawatuma watoto kwenda kushinda  kwenye visima vya maji  wakisha jaza huwafuata.
Watoto hawa sio kwamba wanacheza bali kutokana na shida ya maji kwenye  kitongoji cha mwabagikulu kijiji  cha Ikonongo  kata ya Salawe halmashauri ya wilaya ya Shinyanga  wamekuwa wakitumwa na wazazi wao na kushinda kwenye visima kwaajili ya  kutafuta maji .
KARENY. Powered by Blogger.