MKAMA SHAKENGWA NI KIONGOZI KATIKA KITUO CHA KULELEA WATOTO WENYE ULEMAVU MBALIMBALI CHA BUHANGIJA WAKIWEMO ALBINO. WATOTO
wenye ulemavu wa ngozi katika kituo maalumu cha kulea watoto
hao Buhangija manispaa ya Shinyanga ,wamezidi kuongezeka kituoni hapo
kutokana na wimbi la mauaji y a albino kuibuka tena na kufikia watoto
zaidi ya 100 kupelekwa hapo kutoka maeneo mbalimbali kwa hofu ya
kuuwawa na kufanyiwa ukatili.
Pia watoto wengi wametoka kwenye mikoa ya Tabora,Simiyu na Mwanza
ikiwa watoto wa kike 98 na wakiume 96 , baada ya mauaji hayo
kuibuka tena tangu kwenye mwezi mei mwaka huu kwa kuuwawa mwanamke
mmoja huko mkoani Simiyu na mkoani Tabora watu wawili kuuwawa kwa
kipindi kifupi,ambapo kila siku watoto watatu mpaka wanne wanaletwa
kituoni hapo.
Wakizungumza na waandishi wa habari kituoni hapo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi
misaada iliyotolewa na wadau mbalimbali wa maendeleo, kupitia harambee
iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali Easy flex la mjini Shinyanga kwa
ajili ya kusaidia watoto hao huku mwalimu mkuu wa kituo hicho Peter Ajali
akieleza changamoto za ukosefu wa sehemu ya malazi pia.
Baadhi ya watoto wa kituo hicho wanaosoma shule ya msingi Buhangija
darasa la saba Rehema Masunga,Mkama Shakengwa na D walisema nchi ya
Tanzania inasifika kwa kuwa na amani lakini sasa hali inaelekea kuwa mbaya
kutokana na baadhi ya watu kuwa na roho za kikatili na kuuwa binadamu kama
wanyama .
“Inasikitisha sana kuibuka tena mauaji ya albino tuliona kwenye vyombo vya
habari watu wamekatwa mkono,naiomba jamii iwapuuze waganga wa kienyeji maana
ndiyo wanachangia, tumuamini mungu atatuepusha na unyama huu wa
kikatili”alisema Daniel Limbu.
Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo ambaye pia ni msimamizi wa kituo hicho Peter
Ajali,alisema kufutia kutokea kwa matukio mawili ya albino kukatwa viungo vyao
vya mwili mkoani Tabora na mmoja Bariadi kuuawa matukio hayo
yamesababisha kuongezeka idadi ya watoto kituoni hapo hivyo kuwa na msongamano
mkubwa.
Akizunguma kwenye hafla hiyo meya wa manispaa ya Shinyanga Gulamu Hafidhi
aliitaka jamii kuwa na utamaduni wa kusaidia kituo hicho,badala ya kutegemea
msaada kutoka kwa wafadhili huku akisisitiza mikoa yote iliyopeleka watoto
kutoa michango itakayosaidia kukidhi mahitaji na kuwaomba kuielimisha jamii
umuhimu wa kusaidia.
Awali mkurugenzi mtendaji wa Easy flex production Happness Kihama alisema
changamoto kubwa iliyopo ni uelewa mdogo kwa jamii ,juu ya kusaidia vituo hivyo
vyenye mahitaji maalumu wazee na walemavu kutokana na kukabiliwa na changamoto
mbalimbali ,ikiwa ni pamoja na uchakavu wa majengo,chakula na malazi.
|
0 Response to "WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI WAONGEZEKA KWA KASI KITUO CHA BUHANGIJA KWA HOFU."
Post a Comment