ASKOFU
wa kanisa la EAGT kanda ya magharibi Rafael Machimu
amefikishwa mahakamani na waumini wa kanisa hilo kwa kitendo cha
kumpinga kumfukuza mchungaji wao David Mabushi bila
kutenda kosa lolote jambo ambalo walilieleza ni kwenda kinyume na
taratibu.
Waumini hao wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari walisema
wameamua kumfikisha mahakamani Askofu huyo wakipinga kitendo cha
mchungaji wao na kudai kuwa hakuna kipengele kilichoainishwa cha kumwondoa
mchungaji bila kosa.
“Tumeamua kumfikisha mahakamani askofu Machimu kwa kumwandikia barua ya
kumfukuza mchungaji wetu aondoke katika kanisa letu hivyo tumepinga na
hatujafurahishwa na kitendo hicho ndio maana tukaenda ngazi ya mahakama ili
ikaamue”walisema waumini hao ambao waliomba majina yao yahifadhiwe’alisema
mmoja wa waumini wa kanisa hilo.
Walisema kanisa hilo lilianzishwa mwaka 1992 likiwa chini ya mchungaji John
Chambi ambaye aliondolewa na uongozi wa jimbo la Shinyanga akiwepo mchungaji
Rafael Machimu ambaye wakati huo alikuwa katibu wa jimbo hilo.
Waumini hao walisema toka mwaka huo waliendelea kuabudu bila mchungaji hadi
mwaka 1999 kanisa hilo lilipelekewa mchungaji Mothes Kuzenza ambaye kwa sasa ni
marehemu naye aliondolewa mwaka 2003 katika mazingira ya kutatanisha.
Walisema walivyofuatilia waligundua kuwa ameondolewa kupitia mkono wa Askofu
Machimu ambaye wakati huo alikuwa katibu wa kanda hivyo walidai wamechoka
kuondolewa wachungaji wao mara kwa mara.
“Kwa kweli tumechoka kuondolewa ondolewa wachungaji mara kwa mara tumeamua sasa
kwenda katika ngazi ya mahakama tuone kama mchungaji wetu Mabushi kama atakuwa
na makosa ya kuondolewa katika kanisa la majengo”alisema mmoja wa waumini wa
kanisa hilo.
“Sisi ndiyo waumini wa hilo kanisa na ni waumini wa miaka mingi hakuna mali ya
EAGT hata bati moja haijaleta mali iliyopo humo ni mali ya waumini lakini
kusema aondoke mchungaji aache mali ya EAGT kanisa hilo ni mali ya
waumini”aliongeza.
Aidha kesi hiyo ilianza kutajwa tarehe 4 Agosti mwaka huu katika
mahakama ya hakimu mkazi wa mkoa na mara ya pili ilisikilizwa 14 Agosti ,
ikiwa iliahilishwa kusikilizwa kwa sababu wakili wa mshitakiwa aliiomba
mahakama iahirishe kusikilizwa kutokana na kutoelewa kina cha kesi hiyo hivyo
inatarajiwa kusikilizwa tarehe Agost 25 mwaka huu.
|
0 Response to "WAUMINI WA KANISA LA EAGT WAANDAMANA KUMKATAA ASKOFU WA KANISA HILO."
Post a Comment