Habari za hivi Punde

CHUO KIKUU HURIA KITUO KIPYA CHA SHINYANGA KIMEZINDULIWA,ONGEZEKO LA WADAHILI SERIKALI KUFANYA MIKAKATI.


CHUO kikuu huria huria jana kimezindua  kituo kipya na majengo yake  ambapo sherehe za uzinduzi huo zilifanyika mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mhe. Jenista Mhagama   ambaye ni naibu waziri wa elimu na ufundi  pia mbunge wa jimbo na Peramilo-Songea,na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali  wa mkoa wa   Shinyanga na Simiyu,katika uzinduzi huo kulikuwepo na wahitimu  wa chuo hicho akiwemo mkuu wa mkoa  wa Shinyanga Ally Rufunga na kutunikiwa cheti,hivyo mgeni rasmi huyo alifutahishwa na chuo hicho  kwa kuweza kudahili jumla ya wanafunzi 95,000 nchini wanaochukua masomo kwa mfumo wa masafa marefu huku akiwataka wakazi wa mkoa wa Shinyanga kuchukua fursa  iliyopo na ukaribu wa chuo tofauti na mikoa mingine  na kuwapunguzia gharama ya safari kutafuta elimu hiyo.Baadhi ya wanachuo wanaoendelea na masomo na wale wanao maliza wakisikiliza kwa umakini mkubwa maneno yaliyokuwa yakitolewa na mgeni rasmi ikiwemo viongozi wa chuo hicho.


Makamu wa chuo hicho Pro Tolly  Mbwette  akieleza wageni waalikwa walio kwenye meza kuu na wananchuo kuwa  mfumo wa kupata elimu kwa masafa marefu  umeweza kudahili wanachuo zaidi ya 90,000 nchini   huku ikiwapa fursa ya kuendelea na shughuli zao,lakini kumekuwepo na changamoto katika mfumo huo wa kupotza udahili  na chuo kuamua kuunda uongozi  utakao toa ushauri ,hivyo idadi ya wadahili imezidi kuongezeka  na kuwaomba wananchi wa mkoa wa Shinyanga  kwenda na wakati kwa kupata mafunzo  ya TEHAMA ni muhimu  ili kuendana na utandawazi.


Wakati wa utambulisho ukiendelea  mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose  Nyamubi na mkuu wa wilaya ya Kishapu Wislon Nkhambaku wakiteta jambo kwa kunong'ona wakiwa meza kuu.


Kaimu mkurugenzi wa kituo cha chuo kikuu huria mkoani Shinyanga Agatha Mgogo akisoma taarifa ya chuo hicho mbele ya wageni waalikwa  ambapo alisema kuwa changamoto  ya chuo hicho ni idadi ndogo ya wanafunzi wa kike wanaojitokeza kujiunga na chuo hicho hukua akieleza chuo hicho kilianzishwa mwaka 1994 na kuzinduliwa rasmi mwaka 2000   na jumla ya wanachuo 2168 na waliohai ni 227, hivyo mwaka 2010 kilianzisha  mafunzo ya komputa  na kufanikiwa kuhitimu wanachuo 884 na mpaka sasa  jumla ya wahitimu 334 kwa kozi mbalimbali,pia  ujenzi wa kituo hicho kipya umegahrimu jumla ya shilingi millioni 143.


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose  Nyamubi akiwatambulisha viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga na Simiyu waliofika katika uzinduzi huo.

Mhe.Jenista Mhagama  baada ya kukaribishwa kutoa hotuba yake alikipongeza chuo hicho kwa kupiga hatua kubwa  na kueleza serikali haina budi kukisaidia,alisema vyuo vikuu vya serikali na binafsi  vinavyosimamiwa na TCU vimedahili jumla ya wanafunzi 52,538 ukienda kwenye mfumo rasmi  unaodahiliwa na  TCUni wanafunzi 38,817 ambapo waliokwenye mfumo wa elimu ya ufundi (VETA) kwa kudahili wanafunzi 8656 na vyuo ambavyo haviko  mfumo rasmi wa TCU vimedahili jumla ya wanafunzi 5265  na kuwataka wananchi kujifunza  mifumo iliyopo ili kuweza kubadilisha maisha  na kuwa bora kama zilivyofanikiwa nchi nchingine  kama China na India.


Wanachuo wakitumbuiza kwa nyimbo na mashairi mbele ya mgeni rasmi.

Add caption


Mgeni rasmi akikata utepe  katika ufunguzi wa jengo jipya la chuo kikuu huria lililopo maeneo ya Mwasele kata ya Kambatage manispaa ya Shinyanga.


Mgeni rasmi ambaye ni waziri wa elimu na ufundi mara baada ya kuingia katika uwanja wa jengo hilo huku akiwa na uongozi wa chuo hicho sanajri na viongozi wa mkoa wa Shinyanga na Simiyu.

KARENY. Powered by Blogger.