Habari za hivi Punde

HITILAFU YA UMEME IMESABABISHA MSIKITI WA HINDU KULIPUKA MOTO.



 Kikosi cha zima moto kikifanya juhudi za kuzima moto huo.
MSIKITI wa madhehebu ya Wahindu uliopo maeneo ya Mtaa wa Kibasila karibu na shule ya Olimpia jijini Dar es Salaam, umeteketea kwa moto leo asubuhi ambapo baadhi ya mali zimeungua na mtu mmoja kukimbizwa hospitali kutokana na mshituko.
 Sehemu ya chumba cha msikiti kilichoungua.
Akizungumza na mtandao huu, shuhuda mmoja alisema moto huo umesababishwa na hitilafu ya umeme iliyoanzia kwenye mashine ya luku ambapo baadhi ya waumini walikuwa wakijiandaa  kuupamba msikiti huo.

 Wananchi wakiwa katika eneo la tukio wakisaidia kuokoa baadhi ya mali zilizopo ndani ya msikiti.
 Gari la kikosi cha zima moto likiwa eneo la tukio kuuzima moto.
Baadhi ya waumini wakiwa eneo la tukio.
hivi vitu vilivyo okolewa  ndani ya msikiti ,; HABARI HIYO NI KWA MSAADA WA RICHARD MWAIKENDA BLOG.

0 Response to "HITILAFU YA UMEME IMESABABISHA MSIKITI WA HINDU KULIPUKA MOTO."

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.