Habari za hivi Punde

MAJAMBAZI YAUWA ASKARI WAWILI,WATATU WAJERUHIWA,WALIPUA CHUMBA CHA SILAHA NA KUONDOKA NAZO-USHIROMBO GEITA

KAMANDA WA POLISI MKOANI GEITA JOSEPH  KONYO

BREAKING NEWS;
KITUO  cha polisi kilichopo ushirombo wilayani Bukombe  mkoani Geita  kimevamiwa  na majambazi usiku wa saa tisa kuamkia leo  huku  askari wawili wakiuwawa na watatu wakijeruhiwa  vibaya
Ambapo taarifa za awali  kupitia kwa mwandishi wa blog hii  ametaarifiwa kuwa licha ya matukio hayo  wamelipua  chumba cha kuwekea silaha  na zingine kuondoka nazo,pia wamefanikiwa kuondoka na  bunduki zaidi ya 5  aina ya SMG na kutokomea nazo .
Watu wamekusanyika  kituoni hapo  kushuhudia huku kituo hicho  kikiwa kimezungushiwa   kamba nyekundu kwa kusitisha huduma  na mahabusu  waliokuwemo wamehamishwa.
Hata hivyo kamanda wa jeshi la polisi  mkoani Geita Joseph Konyo yupo katika eneo la tukio kwa uchunguzi zaidi .
Taarifa kamili itaendelea kutolewa kupitia blog hii.

0 Response to "MAJAMBAZI YAUWA ASKARI WAWILI,WATATU WAJERUHIWA,WALIPUA CHUMBA CHA SILAHA NA KUONDOKA NAZO-USHIROMBO GEITA"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.