Mtoto Happiness (10) anayedaiwa kuzua kizazaa mjini Zanzibar.
MTOTO
Happiness (10) (pichani) ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alizua
kizazaa mjini Zanzibar baada ya kuonekana akizungumza na viumbe wa ajabu
na wanyama, ametua jijini Dar kufuatia kufika kisiwani humo
kimaajabu.Kwa mujibu wa mama mzazi wa mtoto huyo, Sarah Zefania, mwanaye
Happiness alianza kuonesha maajabu Zenji tangu alipoonekana kwenye
uwanja wa ndege kisiwani humo wiki iliyopita.
Alisema
maofisa wa uwanja huo walipigwa butwaa baada ya kumwona mtoto huyo
uwanjani amepita sehemu zote za ukaguzi ambazo abiria asiyekaguliwa
nyaraka zake za kusafiria na mitambo maalum ya kuangalia vitu mbalimbali
vikiwemo kemikali hatari, silaha na madawa ya kulevya hawezi kupita.
Kwa
mujibu wa mama huyo, aliambiwa na maofisa wa uwanja huo kuwa sehemu hizo
zote mtoto wake alipita bila kuonekana na kamera za uwanjani hapo wala
kuacha kumbukumbu yoyote hali iliyozidi kuwaumiza vichwa maofisa wa
uwanja huo.
Zefania
alisema wakati maofisa hao wakitafakari hayo, ndipo msamaria mwema mmoja
alijitokeza na kumchukua kwenda kumuhifadhi nyumbani kwake.
Mtoto Happiness akiwa na mama yake mzazi, Sarah Zefania.
“Akiwa
nyumbani kwa msamaria mwema huyo, nimeambiwa mwanangu alianza kumfanyia
maajabu mbalimbali ikiwemo kuzungumza na wanyama na viumbe wengine wa
ajabu au kutoka nje huku mlango umefungwa kwa ndani.
“Kuna
muda alizungumza na viumbe wasioonekana ambapo aliwasiliana nao na
kumletea vitu kadhaa alivyovitaka. Wakati mwingine alizungumza na
wanyama wa mle ndani, kama kuku na paka ambao alikuwa akiwatuma
kumfanyia yote aliyokuwa akiwaagiza.
“Hali
hiyo ilimshtua yule msamaria mwema naye aliomba kupambazuke ili ampeleke
mwanangu ustawi wa jamii. Yaani nahisi pengine angekuwa amemuokota
sehemu bila kukabidhiwa mbele ya mashahidi pengine angemtupa usiku
huohuo.
“Baada ya
kushuhudia vituko hivyo, asubuhi iliyofuata alimkimbiza ustawi wa jamii
ambako nako wameniambia alianza kuwafanyia vituko kama hivyo na
kuwaambia kuwa angewatoroka muda wowote, kisha kuonekana akiparamia juu
ya paa na kutaka kutoka.
“Yaani
kwa muda mfupi waliokaa naye, maofisa wa ustawi wa jamii wanasema
amewahenyesha vya kutosha ndipo walipofanya juhudi za kunitafuta na mimi
nikaenda kumfuata,” alisema mama huyo muda mfupi baada ya kutua
bandarini Dar.
Mtoto Happiness katika pozi.
Paparazi
wetu alipomtaka mtoto huyo kuzungumza alikataa katakata na kujifanya
bubu hali iliyomshangaza hata mama yake. “Nashangaa, sijui kwa nini
hataki kuzungumza na wewe wakati ni mzungumzaji sana,” alisema mama
Happiness.
Akizungumzia
historia ya mtoto huyo, mama huyo alisema alimzalia Musoma, Mara na
mwanaume mmoja aliyemtaja kwa jina la Juli ambaye walitengana na hawana
mawasilino mazuri.
Mama huyo
alisema alimpeleka mtoto wake shuleni lakini kila akifika harudi
nyumbani na kutorokea anakokujua na kuonekana baada ya wiki mbili au
tatu.
Kufuatia
hali hiyo amewaomba wasamaria wema na viongozi wa dini kumwombea mtoto
wake ili arudi katika hali ya kawaida kwani anajua kuna mkono wa mtu wa
karibu uliyemharibu mtoto wake.
0 Response to "MAMA MZAZI WA MTOTO HAPPYNESS ALIA KWA MIUJIZA ANAYOIFANYA MWANAYE KUWA TISHIO."
Post a Comment